Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

258 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Je, unawezaje kutumia ufahamu wa sasa wa Carlos kuhusu Yesu ili kumsaidia kumwelewa Roho Mtakatifu?

Kuongoza Ibada ya Utatu Makanisa mengi ya Kikristo yanafuata Kalenda ya Kanisa, yakitenga siku na majira maalum ili kusisitiza matukio muhimu yaliyomo katika Vitabu vya Injili na Kitabu cha Matendo ya Mitume. Fikiria kama kanisa lako lingekuwa linaadhimisha Jumapili ya Pentekoste* kwa mara ya kwanza kabisa. Katika mapokeo yenu, je, kuna nyimbo, matamko ya baraka, matendo, mapambo, rangi, alama, maandishi, utolewaji wa karama za rohoni, au aina nyingine za ibada ambazo zina msisitizo maalum juu ya Nafsi na kazi ya Roho Mtakatifu? Ikiwa ungewekwa kuwa msimamizi wa ibada hiyo ya Jumapili ya Pentekoste, ni mambo gani ungeweza kupanga ambayo yangelisaidia kusanyiko lako kumwabudu kwa furaha na kumtukuza Mungu Roho Mtakatifu? *Jumapili ya Pentekoste ni Jumapili ya 7 baada ya Pasaka, na kwa kawaida ni ibada inayoadhimisha na kusherehekea kuja kwa Roho Mtakatifu katika kutimiza unabii wa Yoeli (Yoeli 2:28-32) na ahadi ya Yesu (Yohana 14:16-17; 16:7; ; Matendo ya Mitume 1:8). Roho Mtakatifu ni Bwana; Nafsi ya tatu ya Mungu mmoja aliye katika Utatu. Yeye ni nafsi tofauti na Nafsi zingine za Uungu Matakatifu, anafikiri, kutenda, na kupenda kikamilifu kama Baba na Mwana na anashiriki kikamilifu Asili yao ya Uungu. Kama Bwana, anapewa ibada na utukufu pamoja na Baba na Mwana. Roho Mtakatifu ndiye Mpaji wa Uzima: Muumba na Mtegemezaji wa maisha yote. Amewakilishwa kwa isharaa na vyeo katika Maandiko ambavyo hutusaidia kuelewa zaidi kazi yake ya kutoa uzima. Yeye pia ndiye anayetoa uzima mpya (hufanya upya); kwanza kwa njia ya kuzaliwa upya ambapo watu wanafanyika viumbe vipya katika Kristo; na siku moja katika wakati ujao ataizaa mbingu mpya na nchi mpya, makao ya haki. Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili la Nafsi ya Roho Mtakatifu , basi unaweza kuangalia vitabu hivi: Bickersteth, Edward Henry. The Trinity . Grand Rapids, MI: Kregel Publications, 1977.

3

Marejeo ya Tasnifu ya Somo

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Nyenzo na Bibliografia

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker