Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | MUNGU ROHO MTAKAT I FU : NAF S I YA ROHO MTAKAT I FU / 259
Saint Basil. On the Holy Spirit . Crestwood, NY: St. Vladimir’s Seminary Press, 1980. Pia vinapatikana kama vitabu vya kusomea mtandaoni katika tovuti zifuatazo: • www.newadvent.org/fathers/3201000.html • www.monachos.net/patristics/basil/on_holy_spirit_a.shtml Sasa ni wakati wa kujaribu kukazia theolojia hii kwa kuitumia katika huduma halisi. Ni kweli gani kutoka katika somo hili ambazo Mungu amezifunua na kuziangazia kipekee katika moyo wako? Ni hali gani hasa inakuja akilini unapofikiria kuhusu kuwafundisha watu kuelewa fundisho la Roho Mtakatifu? Ni sehemu gani ya somo hili utatumia muda kuitafakari na kuiombea kuelekea juma lijalo. Kutafakari juu ya Nafsi ya Roho Mtakatifu kumekuwa changamoto na kazi ngumu katika historia ya Kanisa. Umeitwa kuingia katika mkondo huu mrefu wa tafakuri ya kitheolojia na kuona matokeo ya kivitendo kwa wale unaowaongoza na kuwafundisha. Kwa bahati nzuri, unaweza kumwomba Roho Mtakatifu mwenyewe aweze kukusaidia kuelewa kweli hizi zenye kina na kukupa mwongozo wa moja kwa moja juu ya namna ambavyo kweli hizi zinapaswa kuathiri maisha na huduma yako. Usiache kumwomba Roho akupe mwanga zaidi juu ya Maandiko ambayo tumejifunza. Ataweka wazi maana na manufaa ya Maandiko hayo. Sala ambayo iko katika sehemu inayofuata inakupa mwanzo mzuri juu ya hili. Roho Mtakatifu wa Mungu, “Unifumbue macho yangu niyaone mambo ya ajabu yaliyomo katika Neno lako.” Ufahamu wangu una mipaka, ufahamu wako hauna kikomo. “Naona kupitia kioo katika giza,” Wewe unachunguza mawazo yake Yeye “anayeishi katika nuru isiyoweza kufikiwa.” Nifundishe maana ya Maandiko uliyoyavuvia. Niangazie akili yangu ili nipate kuijua kweli na kufahamu kile unachotaka nifanye kwa habari ya kweli hiyo. Nipe uwezo wa kutimiza wito wangu wa huduma. Nipe hekima ya kuwaongoza wengine katika maarifa yako ya kweli. Haya yote nayaomba kwa njia ya Yesu Kristo, anayeishi na kutawala pamoja nawe na Baba Mwenyezi, Mungu mmoja, aliyebarikiwa milele. Amina.
Kuhusianisha Somo na Huduma
4
Ushauri na Maombi Ukurasa wa 134 15
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker