Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
UTANGUL I Z I WA FUNGU LA HUDUMA YA K I KR I S TO / 267
Utangulizi wa Fungu la Huduma ya Kikristo
Nakusalimu katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Karibu katika fungu la tatu la Mtaala wa Cornerstone, Huduma ya Kikristo . Kanisa la Mungu katika Yesu Kristo ni mojawapo ya mada zenye kuburudisha na muhimu zaidi katika Maandiko yote. Yesu wa Nazareti, kupitia kifo chake, kuzikwa, na ufufuo wake, ameinuliwa kuwa kichwa juu ya watu wake wapya, wale walioitwa kumwakilisha duniani na kubeba ushahidi wa Ufalme wake uliopo/na utakaokuja. Kuelewa wajibu wa Kanisa katika mpango wa ufalme wa Mungu ni muhimu kwa kila nyanja ya ufuasi binafsi na wa jumuiya; hakuna ufuasi au wokovu nje na tendo la Mungu la kuokoa katika Kanisa na kupitia Kanisa. Kufahamu kile ambacho Mungu anafanya ndani na kupitia watu wake humpa kiongozi wa Mungu uwezo wa kumwakilisha kwa hekima na heshima. Tunakualika kwa shauku kujifunza kuhusu Kanisa ili kufahamu kikamilifu asili ya huduma ulimwenguni leo hii. Katika somo letu la kwanza, Theolojia ya Kanisa : Kanisa katika Ibada , tutautazama wokovu kama msingi wa ibada ya Kanisa. Tutaona kwamba wokovu unakuja kwa neema ya Mungu pekee na kwamba wanadamu kwa namna yoyote ile hawawezi kujipatia au kuustahili kwa jitihada zao binafsi. Kwa hiyo, ibada, ni mwitikio sahihi kwa neema ya Mungu. Bila shaka, Kanisa la Yesu Kristo ni wakala wa Mungu kwa Ufalme wake, na watu wa uwepo wake. Usomaji wako wa nyenzo hii na Neno la Mungu vizae ndani yako upendo wa kina na kujitoa kuishi kwa ajili ya Mungu na kuwajenga wake watakatifu, Kanisa! Viongozi wa Kanisa la Mungu ni zawadi yake ya thamani kwa watu wake kwa vizazi vyote. Ushahidi kwamba Yesu anawapenda upeo watu wake ni kwamba amewapatia mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na walimu ili kuwaandaa watu wake ili wauwakilishe Ufalme wa Mungu katika ulimwengu huu ulioanguka na unaokaribia mwisho (Efe. 4:9-16). Katika somo letu la pili, Misingi ya Uongozi wa Kikristo: Kiongozi wa Kikristo kama Mchungaji , tutajadili mamlaka ya kichungaji, na kuangalia vielelezo na mifano mitatu ya kibiblia ya huduma ya kichungaji: ile ya mlezi, mlinzi na msimamizi, na kiongozi wa kundi la Mungu. Ni vigumu kuiwaza zawadi nzuri zaidi kwa kusanyiko au kikundi cha makusanyiko zaidi ya uongozi wa kimungu, ulio kama wa Kristo, wachungaji wa kweli wanaosimamia na kulinda kundi
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker