Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

268 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

la Mungu. Mungu na atumie somo hili kukuhamasisha kulea na kuwatunza watu wake, kumwiga Mchungaji Mwema aliyetoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake. Tunadhihirisha kujitoa kwetu kwa Mwokozi wetu kwa kutekeleza aina ya uongozi unaomheshimu na kumtukuza Bwana wetu na kuwajenga watu wake. Somo letu la tatu, Kutekeleza Uongozi wa Kikristo : Uongozi Bora wa Ibada linazingatia wazo la uwakilishi wa Bwana Yesu kama msingi katika kutekeleza kila nyanja ya uongozi wa Kikristo kama mawakala na watumishi wake. Sambamba na wazo hili muhimu, pia tutazingatia kwa makini jukumu la kuhudumia Neno na Sakramenti miongoni mwa watu wa Mungu. Ni furaha ilioje kumtumikia Mungu aliye hai kwa kuwatunza watu wake wapendwa! Huduma ya Neno la Mungu ndio moyo hasa wa huduma ya kuwakamilisha watakatifu. Paulo anawaambia Waefeso kwamba Mungu amelipatia Kanisa mitume, manabii, wainjilisti, na wachungaji na walimu ili waweze kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kujenga mwili wa Kristo (Efe. 4:11-12). Hakipo kielelezo popote cha kuliona kanisa kuwa na mhudumu mmoja: kama waamini tunasimamia msimamo wa ukuhani wa waamini wote (1 Pet. 2:8-9), huduma ya jumla ya karama za Roho (1 Kor. 12:1-11), na utendaji wa jumla wa viungo vya mwili wa Kristo (Rum. 12:3-8). Katika somo letu la nne, Huduma ya Kuwakamilisha Watakatifu : Huduma ya Mahubiri , tutaonyesha hatua tatu za kupanga, kuwasilisha, na kufuatilia Neno lililohubiriwa. Kama wawasilishaji wa Neno la Mungu, lazima kwanza tuimarishe mawasiliano na wasikiaji, tuwasilishe ujumbe wa Neno kwa uwazi na kwa ujasiri, na tuoanishe ukweli wa ujumbe na maisha ya wasikilizaji, tukihubiri yote kwa kumtegemea Roho Mtakatifu. Mapinduzi yanaweza kutokea katika huduma ya mijini iwapo wanaume na wanawake walio na vipawa na wanaopatikana wanalitumikia Neno la Mungu katika namna ya kuinua kizazi kipya cha watenda kazi katika jiji – watu wanaoweza kuwajali wanaoumizwa, kuwashirikisha wengine kweli ya Mungu, na kuwatangazia jirani zao Ufalme. Jukumu lako katika huduma hii ni la haraka na lenye kuhitajika. Mungu na abariki jitihada zako unapojitahidi kuongeza uwezo wako wa kujua, kuhubiri, na kufundisha Neno la Mungu lililo hai na la kweli!

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker