Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

UTANGUL I Z I WA FUNGU LA HUDUMA YA K I KR I S TO / 269

Kazi za Kifungu Kama sehemu ya ushiriki wako katika Mtaala wa Cornerstone, utahitajika kufanya uchambuzi (utafiti wa kina) juu ya kifungu kimojawapo katika Neno la Mungu: a. Waefeso 4:1-16 b. Matendo 20:24-28 c. 1 Petro 5:1-4 d. 2 Wakorintho 4:6-12 Kusudi la kazi hii ya ufafanuzi wa Maandiko ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu mojawapo mihimu kuhusu asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya vifungu vilivyopo hapo juu (au andiko ambalo wewe na mkufunzi wako mtakubaliana ambalo huenda halipo kwenye orodha), tunatumai kwamba utaweza kuonyesha jinsi kifungu hiki kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa hali yetu ya kiroho na kwa maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe utambuzi wa jinsi unavyoweza kuhusianisha maana ya kifungu husika moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi wako, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Kukariri Neno ni kipaumbele kikuu katika maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kuna mistari michache, lakini ni ya muhimu katika ujumbe wake. Kila kipindi cha darasa utatarajiwa kukariri mistari uliyopewa na kuiwasilisha kwa Mshauri wako (kwa maneno ya mdomo au kwa maandishi).

Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko

Mistari ya Kukumbuka

a. Waebrania 10:19-22 b. Matendo 20:26-28 c. 1 Petro 2:9-10 d. 2 Timotheo 2:1-2

Kila fungu la mtaala wa Cornerstone limetengewa vitabu vya kiada ambavyo vinapaswa kusomwa na kujadiliwa katika kipindi chote cha kozi. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Cornerstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya sasa ya nyenzo na kazi za usomaji kwa ajili ya fungu hili.

Vitabu vya Kiada

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker