Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 271
Theolojia ya Kanisa Kanisa katika Ibada
S OMO L A 1
Ukurasa wa 141 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kutetea wazo la kwamba wokovu unakuja kwa neema ya Mungu pekee na kwamba wanadamu hawawezi kuupata au kuustahili kwa jitihada zao binafsi. • Kutambua kwamba ibada ni mwitikio sahihi kwa neema ya Mungu. • Kueleza tofauti kati ya maneno “sakramenti” na “maagizo” na kuelezea mtazamo wa kitheolojia ulio nyuma ya kila neno. • Kuelewa maana ya ubatizo na Meza ya Bwana na kujadili tofauti kuu za namna Wakristo wanavyofikiri kuhusu maana zake. Tunaleta Dhabihu za Sifa Soma Warumi 12:1-2 , Waebrania 13:15 , na Habakuki 3:17-19 . Moja ya dhana za kawaida zinazohusiana na mfumo wa ibada za Agano la Kale ni dhana ya dhabihu. Katika ibada ya jumla ya hadhara, kama ilivyoungamanishwa na huduma za hekaluni, wale wanaomkaribia Mungu katika namna hizo zote, walitakiwa kutoa dhabihu, iwe katika nyakati za kawaida za ibada, au hasa katika matukio muhimu kama vile kuwekwa wakfu kwa hekalu. Kwenye wakati huu muhimu, damu ya wanyama ilimwagika sana wakati waabudu wakionyesha shukrani zao kwa Mungu kwa baraka zake kuu katika kusimamishwa kwa nyumba yake (2 Nya. 7:5). Kinachoshangaza sana ni kwamba hakuna mtu aliyepaswa kuja mbele za uwepo wa Mungu bila kumtolea kitu cha kutolewa dhabihu kwa niaba yake. Mungu anastahili matoleo yetu yaliyo bora zaidi, ya juu zaidi, na ya muhimu zaidi, na zaidi hata ya zawadi zetu na vitu vyetu, anastahili nafsi zetu wenyewe. Tunapaswa kumtolea sifa zetu kuu kabisa, sio tu katika nyakati tunapoburudishwa na kuwa na uwezo zaidi, bali hata katika nyakati za magumu na majaribu makubwa zaidi. Mungu wetu hawezi kubadilika; anastahili kuabudiwa pasipo kujali vyovyote mambo yanavyoenda katika maisha na huduma zetu. Ameinuliwa juu ya viumbe vyote, yeye ni Bwana Mungu, anayestahili nguvu zetu, nyimbo zetu bora zaidi, kucheza kwetu kwa kupendeza zaidi,
Malengo ya Somo
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Ibada Ukurasa wa 141 2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker