Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

272 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

huduma yetu kuu zaidi, mwitikio wetu wa nguvu zaidi. Kanisa katika Ibada daima humtolea Mungu dhabihu inayolingana na utakatifu wake na inayostahili kutambulika kwake. Kwa kweli anastahili kuabudiwa, kupewa sifa zetu. Nabii Habakuki anatuangazia njia katika suala la kumtolea Mungu dhabihu ya sifa: Hab. 3:17-19 – Hata kama mitini isipochanua maua, wala mizabibu kuzaa zabibu; hata kama mizeituni isipozaa zeituni, na mashamba yasipotoa chakula; hata kama kondoo wakitoweka zizini, na mifugo kukosekana mazizini, 18 mimi nitaendelea kumfurahia Mwenyezi – Mungu nitamshangilia Mungu anayeniokoa. 19 Bwana, Mwenyezi – Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani. Hebu na tusikilize maneno ya mwandishi kwa Waebrania: Eb. 13:15 – Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Baada ya kukariri na/au kuimba Ukiri wa Nikea (ulio katika Nyongeza), sali sala ifuatayo:

Ukiri wa Nikea na Sala

Mungu wa Milele, Baba yetu, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Wewe peke yako unastahili sifa zote, na kwa sababu hiyo, unahitaji kwamba tukupe heshima na utukufu na sifa. Tunakukaribia kwa jina la Mwanao mpendwa na Mwokozi wetu Yesu Kristo, tukiomba kwamba utujalie nguvu za Roho ili kukutukuza kwa mioyo yetu yote katika ibada ya furaha kwenye mikutano yetu yote, katika mahusiano yetu yote, katika matendo yetu yote, na katika huduma zetu zote. Pokea yote tunayosema na kufanya kama dhabihu inayokubalika ambayo tunaitoa kwako kama Bwana Mungu wetu, ustahiliye sifa na utukufu, katika jina la Yesu tunaomba, Amina.

Pitia upya na mwenzako, andika na/au jikumbushe kifungu cha mstari wa kumbukumbu uliopewa kwenye kipindi cha darasa lililopita: Warumi 8:15-17.

Mapitio ya Kukariri Maandiko Ukurasa wa 142  3

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukabidhi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker