Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 273

KUJENGA DARAJA

Neema Nilisikia hadithi kuhusu mtu ambaye alikuwa akifanya majaribio yahusuyo tabia ya mwanadamu. Mtu huyu alisimama karibu na pampu kwenye kituo cha mafuta katika jiji kubwa na kujaribu kugawa noti za dola ishirini kwa watu waliofika kwenye kituo hicho. Ilimshangaza kuona kwamba hakuna mtu ambaye alichukua zile pesa. Pengine sisi tunaoishi mijini hatushangazwi sana na mwitikio huu. Watu wengi katika majiji makubwa wamejifunza kwa uchungu kwamba “hupati kitu bure” na kwamba mtu yeyote anayeonekana kutoa kitu cha thamani bila malipo huenda si wa kuaminiwa. Sisi wakazi wa mijini tunafahamu kwamba ikiwa kitu kinaonekana kuwa kizuri sana pasipo kasoro ndani yake, basi liko jambo fulani ambalo haliko sawa. Ni kawaida kwetu kuwa na mashaka na vitu vya bure. Somo la leo linahusu ibada kama mwitikio wa neema ya Mungu. Injili ni habari njema ya kwamba kila kitu tunachohitaji na tusingeweza kuwa nacho kinatolewa kwetu na Mungu kama zawadi ya bure ya neema. Kama watu kwenye kituo cha mafuta, pengine wengi wetu hatukutambua kwamba neema ya Mungu ni zawadi ya bure kabisa. Ni lini ulitambua kwa mara ya kwanza kwamba zawadi ya wokovu kamwe haiwezi kupatikana kwa jitihada binafsi bali inakuja tu kama zawadi inayotakiwa kupokelewa? Kwenda Mbali Kupita Kiasi Ikiwa kanisa lako lingetakiwa kujibu swali hili, lingejibuje: “Aina zote za ibada na sifa zimeamriwa kuelekezwa kwa Mungu, lakini kusema ukweli, kujihusisha na (X) kwa namna fulani ni kwenda mbali kupita kiasi. “ Je, katika muktadha wa makanisa yetu, kwenda nje ya mipaka inayokubalika ya namna ibada inavyoeleweka na waumini wa kanisa lako inaweza kumaanisha nini? Je, kuwe na mipaka katika namna tunavyofanya ibada, na ikiwa ndivyo, ni vipi vinapaswa kuwa viwango vya kusimamia mipaka hiyo kwa kuzingatia uhuru wetu katika Kristo, na shauku yetu ya kuonyesha upendo wetu kwa Mungu kwa njia mpya na za kipekee? Liturujia Inachosha Sana – Mungu Anafurahishwa Tukiwa na Huzuni? Wakati wa chakula cha jioni, mmoja wa watoto wa familia fulani ya kanisani alitoa maoni yake kuhusu ibada ya kanisa. Kwa maoni yake ya umri wa miaka 13, ibada za kanisa zilikuwa rasmi sana, zenye kufanana sana, na zenye lugha na shughuli nyingi ambazo hazikuwa na maana yoyote kwake. Alishangaa ni kwa nini hasa nyimbo zilikuwa za zamani sana, na muziki ulikuwa kama wa kwendea mochwari. Mazingira yote yalionekana kuwa ya kusikitisha

1

Ukurasa wa 143  4

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

2

Ukurasa wa 143  5

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker