Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

UTANGUL I Z I WA KAZ I YA K I UKOMBOZ I DH I D I YA UMASK I N I / 29

Utangulizi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

Karibu kwenye mafunzo ya Dk. Alvin Sanders kuhusu dhana ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini. Iwe unafanya kazi ya kujitolea au unahudumu katika huduma ya wakati wote, mafundisho haya yanatoa mtazamo mpya wa jinsi ya kuwawezesha wale wanaoishi katika hali ya umaskini. Njia hii ya kujifunza itakuwezesha kuchunguza mawazo yako kuhusu wale wanaoishi katika hali ya umaskini na jinsi ya kufanya kazi yenye ufanisi miongoni mwao. Mtazamo huu unatoa njia mpya na ya kimapinduzi ya kushirikiana na kuingiliana na wale wanaoishi katika jumuiya zenye mazingira duni, hapa Marekani na duniani kote. Tazama video ya Dk. Don Davis, Fursa ya Kuishi Mtazamo wa Kiukombozi dhidi ya Umaskini , inayozungumzia jinsi tunavyohitaji mtazamo wa wazi, wa kibiblia na wenye mvuto kuhusu maana ya kuendesha huduma yenye kuleta tumaini la maisha katika jumuiya zenye umaskini. Maelezo ya Kozi Kusudi la kozi hii ni kukusaidia ili uweze kufanya aina ya kazi katikati ya jamii maskini ambayo itampa Mungu heshima na kukusaidia kutimiza shauku yako ya kufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri. • Somo letu la kwanza, Tafakari Fupi ya Kitheolojia , linatoa theolojia rahisi na ya vitendo kwa ajili ya kazi ya kupambana na umaskini. Tutazungumza juu ya mada tatu ambazo zinafafanua kwa nini tunafanya kile tunachofanya. • Somo la pili, Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini , linaonyesha aina ya kazi ya kupambana na umaskini ambayo kwa kawaida hutokana na asili yetu ya dhambi. Tutazungumza juu ya kile ambacho kazi yetu itazalisha ikiwa hatuzingatii kujitambua. • Somo la tatu, Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , inafafanua lengo la shughuli zetu. Tutachunguza aina tatu za kazi ya kupambana na umaskini zilizopo na jinsi mwitikio wetu kwa kazi ambayo Kristo amefanya msalabani unapaswa kututamanisha kujielekeza katika ukombozi wa maisha ya watu na mitaa yetu.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker