Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

30 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

• Somo la nne, Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini , linaweka wazi hali ya kiroho ya Mapokeo Makuu ya Kanisa. World Impact inakualika kutendea kazi maarifa haya katika maisha yako kama njia ya kukabiliana na kazi hatarishi ya kupambana na umaskini, na kuyafanya kuwa kichocheo cha kukua katika imani yako. Malengo ya Kozi Baada ya kukamilisha kozi hii ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini, utakuwa na uwezo wa: • Kueleza theolojia fupi ya kibiblia kuhusu kazi ya kupambana na umaskini. • Kuchambua kazi ya kupambana na umaskini na kubaini mazoea na mitazamo yenye sumu (hatarishi). • Kuwa na tafakuri tunduizi na ya kina juu ya kazi ya kupambana na umaskini ili kuioanisha na kazi ya ukombozi ya Mungu katika Kristo. • Kutekeleza dhamira ya kujenga kazi ya kupamana na umaskini katika msingi wa nidhamu thabiti za kiroho ambazo zinawakilisha Mapokeo Makuu ya Kanisa.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker