Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
34 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Tafakari Fupi ya Kitheolojia
Dk. Alvin Sanders
MAUDHUI
Somo hili linatoa theolojia rahisi ya vitendo kuhusu kazi ya kupambana na umaskini. Tutazungumza juu ya mada tatu ambazo zinafafanua kwa nini tunafanya kile tunachofanya. Malengo yetu ya somo hili la Tafakari Fupi ya Kitheolojia ni kukuwezesha wewe: • Kufanya upya fikra na mtazamo wako kuhusu watu wanaoishi katika umaskini. • Kutafakari jinsi mawazo yako ya awali kuhusu wale walio katika umaskini yanahusiana na mada kuu za Biblia. • Kutoa theolojia fupi ya vitendo kuhusiana na kazi ufanyayo ya kupambana na umaskini. Wakristo wana uwezekano mkubwa zaidi kuliko wasio Wakristo kuuona umaskini kama matokeo ya kushindwa kwa mtu binafsi. Mtazamo huu hupelekea walio katika umaskini kuchukuliwa kama “miradi” badala ya watu wa kutumikia, jambo ambalo silo Mungu alilokusudia. Biblia inatoa maagizo muhimu kuhusu jinsi tunavyopaswa kuwatendea walio katika umaskini. Tutachunguza kanuni za Agano la Kale za uwezeshaji na kisha kuangazia mambo mawili tunayoyajua kuhusu Yesu: aliwapendelea maskini, na alionya dhidi ya utajiri.
Muhtasari Ukurasa wa 25 2
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
I. Umaskini ni Mada Inayopatikana katika Agano la Kale na Agano Jipya Kadhalika.
Muhtasari wa Maudhui ya Video
Ukurasa wa 26 3
A. Kanuni za Uwezeshaji za Agano la Kale
Ukurasa wa 27 4
1. Ufafanuzi: Kumwezesha mtu ni kutoa njia za fursa ya kuboresha hali yake.
2. Katika Agano la Kale tunaona kwamba:
a. Uangalifu usio wa kawaida ulipaswa kutolewa katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka kuhusu wale waliokuwa maskini (Kut. 23:6; Am. 5:12; Zab. 10:2, 9).
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker