Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | TAFAKAR I FUP I YA K I THEOLOJ I A / 35

b. Nyakati zote, baadhi ya matunda na mboga zilipaswa kuachwa mashambani ili maskini wakusanye (Law. 19:9-10).

c. Hakuna riba ambayo iliyoruhusiwa kutozwa kwenye mikopo kwa ajili ya wale walioishi katika umaskini (Kut. 22:25).

d. Kila baada ya miaka mitatu zaka ilitolewa kwa yatima na wajane (Kum. 14:28-29).

e. Kila baada ya miaka saba mashamba yalipumzishwa ili yasitumike kwa faida ya wamiliki bali kwa ajili ya wahitaji wapate kuvuna mazao ambayo yaliota yenyewe (Kut. 23:10-11; Law. 25:3-6).

1

f. Watumwa walipaswa kuachiliwa baada ya miaka sita ya utumishi (Kut. 21:2).

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

g. Kila mwaka wa hamsini (Mwaka wa Yubile) ardhi zilipaswa kurejeshwa kwa wamiliki wake wa awali (Law. 25:8-17).

B. Yesu aliwapendelea maskini.

Ukurasa wa 27  5

1. Tunaona namna ambavyo Kristo alionyesha kuwajali kipekee maskini katika huduma yake duniani (Luka 4:18-20).

a. Yesu alifanya huduma yake kama mtu wa maisha ya kawaida (Mk 2:15-17)

b. Mji wa Nazareti alimozaliwa haukuwa na hadhi katika jamii (Yohana 1:44-45).

c. Kuzaliwa kwake katika zizi la ng’ombe ilikuwa tabia ya watu walio katika umaskini (Luka 2:7).

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker