Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | MI S I NG I YA UTUME WA K I KR I S TO : MAONO NA MS I NG I WA K I B I B L I A / 397

• Je, tunapaswa kuzingatia tu mada ambazo watu huzielewa au kuzipenda, au tunapaswa kufundisha mada zote kuu za Biblia, bila kujali lolote? Elezea jibu lako vizuri. • Je, uhusiano wa Israeli na Bwana unalinganaje na uhusiano wako mwenyewe na Bwana? Je, wewe ni kama Waisraeli au uko tofauti nao? Elezea ni kwa namna gani? • Ni kwa nammna gani tunapaswa kufundisha historia ya Israeli kama historia yetu kwa ajili ya maelekezo, kujifunza, na kujenga? (Taz. 1 Kor. 10:6-11: “Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. 10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani”). • Je, lugha ya Biblia kuhusu vita, migogoro, na mapambano inalingana na uzoefu wako mwenyewe kama mwamini? Je, tunapaswa kutumiaje lugha na ishara hizi kwenye maisha yetu wenyewe kama wanafunzi wa Yesu? • Je, kuna aina fulani ya watu ambao hukutamani wamwitikie Bwana? Ina maana gani kwako kwamba Mungu anaweza kumvuta yeyote amtakaye wakati wowote kutoka mahali popote ili awe sehemu ya mwili wake na bibi-arusi wake? (rej. Yn. 6:44). • Je, unajizitama mwenyewe kama askari wa Yesu Kristo, na kama sivyo, kwa nini? Ikiwa taswira hii inakufanya ujisikie vizuri, unafikiri ni kwa nini haifahamiki wala kukubalika zaidi katika ulimwengu wetu leo? • Je, ni jambo la busara kutumia taswira, lugha za picha na ishara za vita leo, pamoja na mizozo yote inayotokea ulimwenguni na wasiwasi wa kimataifa kuhusu ugaidi? Je, tunapaswa kuacha kusisitiza vielelezo hivi ili tusieleweke vibaya na wengine leo? • Je, unaishi kana kwamba unaamini kwamba Ufalme wa Mungu umethibitishwa tena katika uwepo wa Yesu katika Kanisa? Je, unaliona kanisa lako la mahali kama “ishara na kionjo cha Ufalme wa Mungu” duniani leo? Kwa nini ndiyo au kwa nini siyo?

1

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker