Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
398 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
• Kamilisha sentensi ifuatayo: “Kama kungekuwa na jambo moja tu ambalo ningeweza kufanya sasa hivi ili kuzifanya mada na taswira hizi ziwe hai maishani mwangu, mahali nilipo, jambo hilo lingekuwa . . .”
MIFANOHALISI
Taswira za Vita Hazijengi Imani Ijapokuwa Biblia imejaa lugha za picha, taswira, mifano, na mtiririko wa hadithi za vita za ulimwengu, za Yehova kama shujaa, na Kristo kama Mshindi mkuu juu ya Shetani, kifo, laana, na nguvu, Wakristo wengi wa kisasa wanahisi wasiwasi juu ya mambo hayo. Katika ulimwengu unaokumbwa na ugaidi, mizozo, na vita, Wakristo wengi wa kweli hawaamini kwamba taswira na mitazamo ya namna hiyo ni ya muhimu. Badala ya kujikita kwenye moyo wa Injili, upendo wa Mungu ulioonyeshwa katika kifo cha Yesu Kristo kwa ulimwengu, taswira kama hiyo ya vita inachanganya watu, inaingiza mawazo ambayo ni magumu kueleweka ulimwenguni leo, na ambayo yanaweza hata kufifisha picha ya jumla ya Huruma ya Mungu kwa maskini na walioonewa. Wakristo wengine (ambao pia ni halisi na wa kibiblia) wanahisi kwamba kupuuza au kudharau msisitizo wa kibiblia juu ya vita vya kiroho pengine ni kupoteza mada na taswira muhimu zaidi katika kuuelewa ulimwengu wa kiroho kama unavyoelezwa katika Maandiko. Hawa wanaoona thamani ya taswira za vita wanathibitisha kwamba hatupigani na wanadamu, bali tunapigana dhidi ya zile mamlaka ambazo zinapambana kutuangamiza: “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” (Efe. 6:12). Mada hizi zinatupatia ufahamu mkubwa juu ya ulimwengu wa mapambano ya Kikristo kwa habari ya wema dhidi ya uovu, na tunapaswa kujifunza kupitia taswira hizo. Ni lipi kati ya makundi haya liko sahihi katika kuwasilisha asili ya imani ya Kikristo katika ulimwengu wa leo: je, tunapaswa kutafuta taswira nyingine za kuelewa na kuwasilisha imani katika ulimwengu ulioharibiwa na vita na migogoro, au tunapaswa kuzitumia hizi hizi ili wengine waweze kuelewa vizuri zaidi asili ya vita hii, na kwa nini ni muhimu kwao kuelewa na kutumia taswira hizi katika maisha yao? Mitindo ya Kiroho ya Maeneo ya Nje ya Miji dhidi Ile ya Maeneo ya Mijini Kuhusiana na mada ya vita katika ufuasi na umisheni wa Kikristo, mtu anaweza kuona tofauti kubwa kati ya mitindo ya kiroho na vita ya mijini na nje ya miji. Tukizungumza kwa ujumla, kwa wakazi wengi wa wa nje ya miji ambao wamepata kiasi fulani cha utajiri na wepesi, mkazo mkubwa katika safari yao ya kiroho ni usalama na ulinzi. Mara nyingi jamii huchukuliwa kama nguvu ovu inayopinga
1
Ukurasa wa 175 3
1
U T U M E K A T I K A M I J I
2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker