Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | MI S I NG I YA UTUME WA K I KR I S TO : MAONO NA MS I NG I WA K I B I B L I A / 399

maadili na heshima katika familia, na lengo ni kutunza maadili haya na mifumo ya imani ili kuhakikisha kwamba familia na mitaa inakuwa salama dhidi ya nguvu hizo ambazo zingetaka kudhoofisha usalama huo. Kwa upande mwingine, mitindo ya kiroho ya mijini inajikita kwenye migogoro na mapambano na ulimwengu na mawakala wake. Vita vinatazamwa kama mwitikio wa lazima dhidi ya uovu uliopo kila mahali unaotaka kuwaangamiza. Matarajio ya Mkristo mkomavu yatakuwa ni uangalifu wa mara kwa mara na kujihusisha kwenye mapambano ya kujitahidi kuzishinda nguvu hizi kila siku. Mawazo makuu hapa hayajajengwa katika kuhifadhi maadili, bali kuwakomboa watu kutoka kwenye mifumo dhalimu na ya hatari inayowashikilia. Wakiwa hawana chochote cha kulinda na hawana utajiri wa kuhifadhi, wana mwelekeo wa kuzishikilia mada na taswira za kiroho ambazo zinasisitiza mapigano, kukabiliana, na mapambano. Je, unauzungumziaje utofauti wa mitindo hii – je, ni matokeo tu ya safari za kiroho kulingana na utofauti wa mazingira, au kuna jambo la msingi zaidi katika mawazo tofauti na utendaji kazi wake katika maisha ya kiroho? Je, Ukristo ni Dini ya Magharibi? Kwa bahati mbaya, wengi wamehusisha kimakosa maisha ya Kikristo na aina ya mfumo wa udhibiti wa Ulaya ambao unautazama Ukristo kama imani ya Magharibi, ya wazungu wa tabaka la kati. Ijapokuwa vuguvugu kubwa zaidi la Kikristo kwa sasa linapatikana katika ulimwengu wa tatu na linahusisha watu ambao si wazungu, vitovu vya nguvu na fedha kwa sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kikristo bado ni vya wazungu na watu wa magharibi. Seminari nyingi, makampuni ya uchapishaji, na makanisa na mashirika mbalimbali ya kiimani yanaendeshwa na watu wa Ulaya au wenye asili ya Amerika Kaskazini, ambao kwa kawaida ni wazungu, na ndio wenye mtandao wa nguvu na rasilimali. Kwa sababu hiyo, kwa watu wengi walio nje ya imani hii, Ukristo hauonekani kama watu wapya wa Mungu waliojengwa juu ya imani jumuishi, usawa, utofauti, na umoja – wa mataifa mengi na wa tamaduni nyingi, wakifurahia kifungo kimoja katika Roho. Badala yake, mwili na bibi-arusi wa Kristo unaonekana kuwa wenye mwelekeo wa Wamataifa, na utawala wa kimagharibi. Mawazo haya yanadhoofisha uwezo wetu wa kuingia katika jamii fulani, ambazo zinauona Ukristo kama dini ya kimagharibi kitamaduni; mataifa mengi hayako wazi tena kupokea wamishenari wa Kikristo, wakiwaona kama mawakala wa maadili na kanuni za kimagharibi, si wawakilishi wa raia wa mbinguni. Huku pakiwa na ongezeko la chuki dhidi ya Ukristo na umagharibi, sisi kama viongozi wa umisheni tunapaswa kufikiria vipi kuhusu kizazi kijacho cha kumjulisha Kristo katika tamaduni mbalimbali, hasa zile ambazo zina mashaka na hazina imani na chochote cha kimagharibi na cha kizungu?

1

U T U M E K A T I K A M I J I

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker