Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

400 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Mada ya utume kama Vita vya Milki pengine ndiyo mada yenye nguvu zaidi ya umisheni katika Maandiko, na huanza na utawala mkuu wa Yehova Mungu kama muumbaji na mtegemezaji wa vitu vyote. Utawala wa Mungu ulipingwa katika uasi wa fumbo la uovu (yaani, uasi wa kishetani huko mbinguni), ambao ulisababisha majaribu na anguko la mwanadamu, na laana juu ya uumbaji. Mungu aliweka uadui kati ya Uzao wa mwanamke na nyoka, na kwa uwezo na fadhili zake akaahidi kukomesha uasi huo kupitia Uzao wa mwanamke. Kama matokeo ya Anguko, ulimwengu uko vitani na Mungu amejitangaza kuwa anapigana na nyoka na wale walio upande wake. Mungu alijidhihirisha kuwa shujaa wa kiungu katika pambano lake dhidi ya uovu uliofananishwa na mto na bahari, ushindi wake dhidi ya Farao na majeshi yake, na mataifa ya Kanaani. Hata hivyo, Mungu pia alilazimika kupigana na watu wake mwenyewe kwa sababu ya kutotii na uasi wao. Kwa kuongezea, manabii wa Israeli walimuelezea Mungu kama shujaa wa kiungu ambaye hatimaye kupitia Masihi wake angeharibu uovu wote mara moja na kwa zote. Utawala huu wa Kimasihi umeanzishwa kupitia nafsi ya Yesu, ambaye katika kuzaliwa kwake, mafundisho, miujiza, kuondoa pepo, matendo, kifo, na ufufuo wake ameleta Ufalme wa Mungu katika uhalisia. Ufalme “tayari upo” na “bado utakuja;” tayari umekuja katika utimilifu wa Yesu kama ahadi ya Kimasihi lakini utakamilika katika Kuja kwake Mara ya Pili. Leo katika ulimwengu huu na katika zama zetu, Kanisa la Yesu Kristo ni ishara na kionjo cha Ufalme uliopo, unaokaliwa na Roho Mtakatifu, dhamana ya urithi kamili. Sasa kanisa kama wakala na msaidizi wa Yesu Kristo limepewa mamlaka ya kutangaza na kudhihirisha ushindi wa Kristo dhidi ya Shetani na laana. Utume unatangaza kwamba Mungu kwa sasa anaimarisha utawala wake leo juu ya ulimwengu wake katika Yesu Kristo, na kupitia wakala wake, Kanisa. Ikiwa ungependelea kufuatilia baadhi ya mawazo ya Maono na Msingi wa Kibiblia kwa Umisheni wa Kikristo , unaweza kuhitaji kujaribu vitabu hivi: Costas, Orlando E. Christ Outside the Gate: Mission Beyond Christendom . Maryknoll, NY: Orbis Books, 1982. Curtis, Brent, and John Eldredge. The Sacred Romance: Drawing Closer to the Heart of God. Nashville: Nelson Books, 1997. Jones, E. Stanley. Is the Kingdom of God Realism? New York: Abingdon-Cokesbury, 1940. Newbigin, Lesslie. Sign of the Kingdom . Grand Rapids: Eerdmans, 1980.

Marudio ya Tasnifu ya Somo

1

U T U M E K A T I K A M I J I

Nyenzo na Bibliografia

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker