Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | MI S I NG I YA UTUME WA K I KR I S TO : MAONO NA MS I NG I WA K I B I B L I A / 401
Yoder, John Howard. The Politics of Jesus . Grand Rapids: Eerdmans, 1972.
Mwombe Mungu Roho Mtakatifu akusaidie kutafakari juu ya mada zinazozungumziwa katika somo hili ili upate kuzihusianisha kwa namna ya kivitendo katika maisha na huduma yako mwenyewe. Chagua mawazo na mada moja muhimu au zaidi ya kuitafakari na kuiombea katika wiki hii yote ijayo, na uwe wazi kwa uongozi wa Roho kuhusu njia mahususi unazoweza kuelewa vyema na kutumia maana ya mada hizi kwenye mafundisho, mahubiri, na ushuhuda wako. Kwa pamoja na wanafunzi wenzako, mtafuteni Bwana katika kuombeana na kuombea mambo ambayo Mungu ameyafunua katika somo hili. Pia, weka ahadi ya kutumia muda mrefu wa maombi pamoja na Bwana, peke yako na ikiwezekana pamoja na wengine wakati wa wiki. Muda mrefu wa maombi ni ufunguo wa matumizi ya kweli za Neno na mabadiliko ya maisha ya mtu mbele za Bwana. E. M. Bounds anaweka jambo hili wazi: Ingawa sala nyingi za faragha, katika uhalisia wa mambo, lazima ziwe fupi; wakati sala za umma, kama zilivyo taratibu, zinapaswa kuwa fupi; wakati kuna nafasi ya kutosha kwa ajili ya sala fupi na thamani katika hizo – bado katika ushirika wetu wa faragha na Mungu wakati ni kipengele muhimu chenye thamani yake. Kutumia muda mwingi pamoja na Mungu ndio siri ya maombi yote yenye mafanikio. Maombi yanayoonekana kama nguvu kuu ni matokeo ya haraka ya kutumia muda mwingi pamoja na Mungu. Sala zetu fupi zinapata maana na ufanisi wake kutoka kwenye zile ndefu zilizotangulia. Sala fupi yenye ushindi haiwezi kuombwa na mtu ambaye hajashinda pamoja na Mungu katika pambano kuu na endelevu zaidi. Ushindi wa imani wa Yakobo haungeweza kupatikana bila pambano lile la usiku kucha. Ufahamu wa Mungu huwa hauitwi kwa wito wa ghafla. Mungu huwa hatoi karama zake kwa watu wa kawaida wanaokuja na kuondoka kwa haraka. Muda mwingi na Mungu pekee ndiyo siri ya kumjua. Huonekana kwa wenye imani isiyokoma wamjuao. Yeye huwapa zawadi zake nyingi sana wale ambao wanaonyesha shauku na shukrani zao kwa zawadi hizo kwa njia ya bidii na ustahimilivu wao. Kristo, ambaye katika hili na mambo mengine ni Mfano wetu, mara nyingi alitumia usiku mzima katika maombi. Kawaida yake ilikuwa kuomba sana. Alikuwa na mahali pake pa kawaida pa kusali. Vipindi vingi virefu vya kuomba vilitengeneza historia na tabia yake. Paulo aliomba mchana na usiku. Ilimbidi Danieli kuchukua muda kutoka katika shughuli nyingi na muhimu sana ili kuweza kusali mara tatu kwa siku. Maombi ya Daudi ya asubuhi, mchana, na usiku katika vipindi
Kuhusianisha Somo na Huduma
Ushauri na Maombi Ukurasa wa 176 4
1
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker