Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

402 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

mbalimbali, bila shaka yalikuwa ya muda mrefu sana. Ingawa hatuna simulizi kamili kuhusu muda ambao watakatifu hao wa Biblia walitumia katika maombi, dalili zinaonyesha kwamba walitumia muda mwingi katika maombi, na katika nyakati fulani vipindi virefu vya maombi vilikuwa kawaida yao.

~ E. M. Bounds. Power Through Prayer. (toleo la kielektroniki). Oak Harbor, WA: Logos Research Systems, 1999.

Katika fungu hili lote, jitoe kuomba kwa muda mrefu juu ya moyo wako mwenyewe, mahitaji ya wanafunzi wenzako, na maombi ya wazi kwa Bwana kuhusu uongozi wake na kweli hizi katika maisha yako.

KAZI

Mathayo 28:18-20

Kukariri Maandiko

1

U T U M E K A T I K A M I J I

Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kujua kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize Mshauri wako.

Kazi ya Usomaji

Soma maeneo uliyoagizwa na uandike muhtasari usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo moja. Katika muhtasari huu tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika kila eneo husika la usomaji. Huhitaji kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali kabidhi muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Tafadhali ona “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kwenye ukurasa wa 16). Somo letu linalofuata, Uinjilisti na Vita ya Rohoni: Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu , linaonyesha kwamba kwa njia ya maisha, kifo, na ufufuo wa Yesu Kristo, waamini wanakombolewa kutoka kwenye utawala wa Shetani, na pia kutoka kwenye athari za laana kupitia nguvu ya Roho. Uinjilisti ni kutangaza kwa ulimwengu wote ule ukombozi wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Bwana wetu Yesu anatamani kwamba tuzae matunda mengi kwa utukufu na sifa ya Mungu (Yohana 15:8-16). Bwana na abariki kujifunza kwako Neno lake ili uweze kujiunga na wavunaji katika kukusanya matunda ya wokovu wa Bwana mwenyewe, kwa utukufu wa Baba!

Kazi Zingine

Kuelekea Somo Linalofuata

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker