Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | U I NJ I L I S T I NA V I TA YA ROHON I : KUFUNGWA KWA MTU MWENYE NGUVU / 405
Uinjilisti na Vita ya Rohoni Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu
S OMO L A 2
Ukurasa wa 177 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuonyesha kutoka katika Biblia kwamba kimsingi wokovu ni tendo la Mungu, kwa nguvu za Roho Mtakatifu, kumkomboa mwanadamu na uumbaji wake kutoka katika utawala wa Shetani na udhalimu na hofu ya kifo, na pia dhidi ya athari za laana na dhambi. • Kuelezea kwa uwazi namna uinjilisti unavyotangaza kwa ulimwengu wote ukombozi wa Mungu ulioahidiwa na kutabiriwa, kwa njia ya Yesu Kristo katika uwezo wa Roho Mtakatifu. Kama Sisi Ili Kutukomboa Ebr. 2:14-15 – Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. Pengine hakuna wazo lolote katika Maandiko linaloweza kulinganishwa na unyenyekevu usio wa kawaida wa Bwana wetu Yesu katika nia yake ya kuwa kama sisi ili kutukomboa. Andiko hili linadokeza kwamba Bwana Yesu, katika unyenyekevu na utii wake mkuu kwa Baba katika kule kufanyika mwili, alishiriki asili yetu, yaani, mwili na damu yetu, ili kwa njia ya mauti amwangamize yeye aliye na nguvu za mauti juu ya wanadamu, shetani. Hatutawahi kujua kina cha unyenyekevu na kujikana kilichohusika katika tendo hili kuu la wema na neema kwetu. Kwa sababu ya utumwa tuliokuwa nao kwa sababu ya dhambi zetu wenyewe, Bwana wetu aliamua kuwa kama sisi, kushiriki udhaifu wetu, kushiriki katika mambo yale yale tunayofanya, ili avunje kitanzi cha kifo juu yetu, na kutuweka huru kwa kusudi la Bwana mwenyewe na hatima yetu mpya. Mtu yeyote asifikirie kwamba mapambano au maumivu yake mwenyewe ni ya kipekee au kwa namna fulani ni ya kupita kiasi au nadra sana kiasi kwamba hata Bwana hawezi kuhafahamu kabisa uchungu wake. Andiko hili linayatuliza mawazo yote tuliyo nayo kuhusu upekee wa mapambano yetu. Yesu mwenyewe alifanyika
Malengo ya Somo Ukurasa wa 177 2
2
U T U M E K A T I K A M I J I
Ibada Ukurasa wa 177 3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker