Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
406 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
kama sisi ili atukomboe sisi ambao, maisha yetu yote, tulikuwa chini ya nguvu za dhambi na matokeo yake yasiyoepukika, yaani kifo. Sifa ni kwa Yeye ambaye alikuwa tayari kushiriki katika utu wetu ili kuvunja utumwa wetu.
Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Ee Mungu, ambaye Mwana wako mbarikiwa alikuja ulimwenguni ili azivunje kazi za Ibilisi na kutufanya watoto wa Mungu na warithi wa uzima wa milele: Kwa tumaini hili, utujalie, kujitakasa kama yeye alivyo safi, ili wakati anakupoja tena na uwezo na utukufu mkuu, tupate kufanywa kama yeye katika ufalme wake wa milele na utukufu; anapoishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
~ Presbyterian Church (USA). Book of Common Worship . Louisville, KY: Westminister/John Knox Press, 1993. uk. 236.
2
Pitia upya na mwenzako, andika na/au jikumbushe kifungu cha mstari wa kumbukumbu uliopewa kwenye kipindi cha darasa lililopita: Mathayo 28:18-20.
Mapitio ya Kukariri Maandiko
U T U M E K A T I K A M I J I
Wasilisha muhtasari wako wa kazi ya kusoma ya juma lililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache ya mambo makuu ambayo waandishi walikuwa wakitafuta kuyaainisha katika kazi ya usomaji uliyopewa (Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
KUJENGA DARAJA
“Kwa Nini Mambo Mabaya HuwapataWatuWema?” Jioni moja, mtoto mdogo alikuwa akitazama taarifa ya habari pamoja na ndugu zake. Katika kusikiliza taarifa hizo kituo kilisimulia kisa cha kijana mdogo aliyeuawa kwa bahati mbaya na dereva aliyeshindwa kudhibiti gari lake na kujikuta amemgonga kijana huyo ambaye alifariki dunia kutokana na majeraha hayo muda mfupi baadaye. Baadaye usiku huohuo, akiwa amejawa na udadisi na maswali mengi juu ya tukio hilo, binti huyu mdogo alimuuliza mama yake aliyeamini, “Mama, unakumbuka habari tuliyosikia muda si mrefu, mvulana aliyegongwa na kuuawa na gari? Kwa nini jambo lile lilitokea? Kwa nini mambo kama hayo hutokea kwa watu, hata kwa watu ambao hawajafanya lolote baya? Je, Mungu hawezi
1
Ukurasa wa 178 4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker