Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | U I NJ I L I S T I NA V I TA YA ROHON I : KUFUNGWA KWA MTU MWENYE NGUVU / 407
kuzuia mambo kama hayo kutokea? Kwa nini mambo mabaya huwapata watu wema?” Ungejibuje swali la msichana huyu mdogo kama ungekuwa mzazi wake?
“Hakuna Ibilisi.” Katika mazungumzo kazini, wakati wa chakula cha mchana, mabishano madogo yanazuka katika chumba cha chakula cha mchana kati ya wafanyakazi wenzako wawili. Katika kuzungumzia matukio ya Septemba 11, uharibifu wa kutisha wa Trade Towers katika Jiji la New York, mfanyakazi mmoja anadai kwamba tukio hili na mengine kama hayo ni kazi ya watu waovu ambao wanatumiwa na ibilisi. Uongo wa shetani ndio chanzo cha uovu wote duniani. Mfanyakazi mwingine anakataa dhana hiyo, akisema kwamba uovu ni matokeo ya uchaguzi mbaya wa watu binafsi na hauhusiani na aina yoyote ya ushiriki wa kipepo au wa kishetani. Alisema, kumlaumu Shetani kwa mambo mbalimbali, ni kisingizio tu cha kutokuwajibika kibinafsi kwa vitendo vya mtu mwenyewe. Wakionekana kutofika popote katika mjadala wao, wanakugeukia na kukuomba maoni yako. Je, ungewaambia nini kuhusu suala hilo? “Unaweza Kuniahidi Nini?” Katika kumshirikisha rafiki yake imani yake shuleni, mwanafunzi mmoja wa Yesu aliyekuwa mchanga bado alitoa muhtasari wa habari njema ya wokovu wa Mungu kupitia Yesu Kristo. Alieleza Yesu alikuwa nani, kwa nini alikuja duniani na kufa, na Mungu anaahidi nini kwa wale wanaompokea Yesu kuwa Bwana na kuamini kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Baada ya kusikiliza kwa utulivu kwa muda ushuhuda huu wa Injili, kijana mmoja aliyekuwa akitafuta kukata shauri alisema, “Hilo limekaa vizuri, lakini sidhani kama wazo la uzima wa milele na wokovu na mengine ya jinsi hiyo yana msaada kwangu kwa sasa. Sina fedha, nilipoteza kazi yangu siku mbili zilizopita, na kodi ya nyumba inatarajiwa kwisha baada ya wiki mbili. Nilifeli somo la Kiingereza kwenye mtihani wangu wa muhula, na mimi na rafiki yangu wa kike tunahangaika sana. Sioni namna kumwamini Yesu kutakavyobadilisha maisha yangu hata kidogo. Ninataka kwenda mbinguni nitakapokufa, lakini vipi kuhusu leo, vipi kuhusu sasa hivi? Unaweza kuniahidi nini, maisha yangu yatabadilikaje nikisema “ndiyo!” kwa Yesu leo? Je, hilo litaleta mabadiliko yoyote halisi katika maisha yangu leo hii?” Je, yule mwanafunzi mchanga anawezaje kujibu swali hili?
2
2
U T U M E K A T I K A M I J I
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker