Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
408 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Vita ya Kiroho: Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu
Mch. Dk. Don L. Davis
MAUDHUI
Wokovu ni tendo la Mungu kumkomboa mtu kutoka katika mikono ya shetani na athari za Anguko, yaani, kutoka katika dhambi na utawala wake. Uinjilisti ni tangazo la habari njema za ukombozi na wokovu huu wa kutolewa kwa Shetani na kwenye dhambi, wokovu ambao Mungu ameukamilisha kwa ajili yetu kwa njia ya Yesu Kristo. Lengo letu katika somo hili, Vita ya Kiroho: Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Biblia inafundisha kwamba wokovu ni tendo la Mungu kumkomboa mwanadamu na uumbaji kutoka katika nguvu za shetani na matokeo ya dhambi. • Kupitia imani katika Yesu Kristo, wale wanaoamini wanaweza kukombolewa kutoka chini ya utawala wa Shetani na kutoka katika udhalimu wake (udanganyifu na ukandamizaji wake) na hofu ya kifo. • Wokovu wa Mungu katika Kristo pia huwakomboa wale wanaoamini dhidi ya athari za laana na dhambi kwa nguvu za Roho Mtakatifu. • Uinjilisti ni tangazo la ukombozi wa Mungu kwa ulimwengu wote, ukombozi ulioahidiwa na kutabiriwa kwa njia ya Yesu Kristo katika uwezo wa Roho Mtakatifu.
Muhtasari Ukurasa wa 178 5
2
U T U M E K A T I K A M I J I
I. Wokovu Ni Ukombozi Kutoka katika Nguvu za Ibilisi.
Muhtasari wa Maudhi yaVideo
A. Kusudi la umwilisho: kuharibu kazi za shetani
1. Alidhihirishwa ili kuharibu kazi za Ibilisi, 1 Yoh. 3:8.
2. Yesu aliwavua silaha watawala na mamlaka, Kol. 2:15.
3. Alishiriki asili yetu ili kumwangamiza ibilisi aliyekuwa na nguvu za mauti, Ebr. 2:14.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker