Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MKAZO KUHUSU UZAZ I : UKUA J I WA KAN I SA / 429

3. Unda vikundi vidogo vidogo, mafunzo ya Biblia, n.k. ili fuatilia waumini wapya, endelea na uinjilisti, na kutambua na kuwafunza viongozi wanaoibuka.

4. Tangaza kuzaliwa kwa kanisa jipya mtaani na kukutana mara kwa mara kwa ajili ya ibada, mafundisho na ushirika.

D. Hatua ya Nne: Lea – kupitia vikundi vidogo na mafunzo ya mtu binafsi, imarisha wanafunzi wa Yesu katika misingi ya maisha ya Kikristo, jumuiya ya Kikristo, na ukuaji wa kanisa .

1. Maandiko muhimu

a. 1 The. 2:5-9

b. 1 Kor. 4:14-15

3

2. Kanuni ya msingi: kupitia vikundi vidogo na urafiki wa kibinafsi, ibada ya pamoja, na mafundisho thabiti na ushirika, waamini wapya wanalelewa na kujengwa ili waweze kuishi kama wanafunzi wa Yesu katika mwili wa Kristo.

U T U M E K A T I K A M I J I

3. Kuza ufuasi wa mtu binafsi na wa kikundi.

4. Jaza nafasi muhimu za uongozi katika kanisa: tambua karama za rohoni na uzitumie.

III. Wezesha: Waingize Kazini Viongozi kwa ajili ya Kanisa na Wafundishe Kujizalisha. Mdo. 20:28 – Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker