Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

480 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

K I A M B AT I S H O C H A 5 Sampuli ya Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko

Jina: ___________________________________ Maksi: _______________________

Tafsiri: _______________________ Andiko Lililokaririwa: _______________________

Ni wajibu wa mwanafunzi kuweka alama ya Kazi yake ya Kukariri Maandiko. Kama ukumbusho, tafadhali kariri Maandiko kutoka katika tafsiri pekee (km. BHN, SUV, NEN, n.k.) na si Biblia za mafafanuzi (mfano The Living Bible, The Message). Tafadhali fuata utaratibu ulio hapa chini ili kusahihisha kazi yako: 1. Weka mbali visaidizi vyovyote unavyoweza kuwa navyo (pamoja na Biblia yako), na kwenye karatasi tupu, andika kifungu chako cha Kumbukumbu ya Maandiko kwa ukamilifu.

2. Andika tafsiri ya Biblia uliyotumia pamoja na jina lako juu ya ukurasa wako.

3. Kwa kutumia Biblia yako, kagua kazi yako, neno kwa neno, na uweke mstari katika makosa yoyote ambayo unaweza kuwa umeyafanya katika uandishi wako.

Yafuatayo yanahesabiwa kama makosa: • Neno lisilo sahihi

(kila neno lisilo sahihi ni kosa) • Neno lililokosekana (kila neno lililokosekana ni kosa) • Neno au maneno yaliyoandikwa nje ya mpangilio (kila neno lisilo katika mpangilio ni kosa)

4. Hesabu idadi ya makosa na kisha uandike idadi hiyo hapa: _______

5. Kifungo cha Maandiko ulichokariri kina mistari mingapi? _______

6. Unaruhusiwa jumla ya kosa moja kwa kila mstari kupata alama kamili kwa kazi yako ya kumbukumbu ya Maandiko. Ikiwa kifungu chako kilikuwa mistari mitatu na ukapata alama kamili katika mistari miwili na ukawa na makosa matatu katika mstari wa tatu, utapata alama zote kamili za kifungu husika. 7. Unaruhusiwa jumla ya makosa mawili kwa kila mstari kupata nusu alama kwa kifungu. Ikiwa kifungu chako kilikuwa mistari mitatu na ulifanya makosa 4-6 utapata nusu ya alama zote za kifungu husika.

Yafuatayo HAYAPASWI kuhesabiwa

kama makosa: • Kukosekana kwa uakifishaji au uakifishaji usio sahihi • Neno lililoandikwa vibaya au kukosewa

8. Ikiwa ulifanya zaidi ya makosa mawili kwa kila mtari, hutapokea alama yoyote kwa kifungu hiki.

9. Andika “alama kamili,” “nusu ya alama,” au “hakuna alama” juu ya ukurasa huu, kulingana na jinsi ulivyofanya kazi yako, na kabidhi fomu hii kwa mwalimu wako.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker