Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
V I AMBAT I SHO / 481
A P P E N D I X 6 Namna ya Kuandika Kazi Yako Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Kazi za Marejeo. The Urban Ministry Institute
Wizi wa kazi hutokea pale unapotumia mawazo ya mtu mwingine kana kwamba ni ya kwako bila kuwapa heshima wanayostahili. Katika kazi za kitaalamu ni kosa kuiba mawazo ya mtu mwingine, kama tu ilivyokosa kuiba mali ya mtu mwingine. Mawazo haya yanaweza kuwa ni kutoka kwa mwandishi wa kitabu, chapisho ulilolisoma au kutoka kwa Mwanafunzi mwenzako. Njia nzuri ya kuepuka hili ni kutumia kwa umakini “maelezo” (maelezo ya ziada yaani [textnotes] , maelezo ya chini [footnotes] , maelezo ya mwisho [endnotes] , n.k.) na kipengele cha “Kazi Zilizonukuliwa” ili kuwasaidia wale wanaosoma kazi yako kujua kama wazo hilo wanalolisoma ni la kwako au umeliazima kutoka kwa mtu mwingine. Nukuu za marejeo zinahitajika katika chapisho kila unapotumia wazo au taarifa ambayo inatoka kutoka kwenye kazi ya mtu mwingine. Nukuu za marejeo zinahusisha sehemu mbili: • Madokezo ndani/katikati ya andiko lako (kazi yako) yanayowekwa kila baada ya nukuu ambayo inatoka katika chanzo cha nje. Kuna aina kuu tatu za maelezo: Maelezo katika mabano (parenthetical notes) , maelezo ya chini (footnotes) , na maelezo ya mwishoni (endnotes) . Katika taasisi yetu ya The Urban Ministry Institute, tuna shauri mwanafunzi atumie maelezo katika mabano. Maelezo haya yanaonyesha jina la mwisho la mwandishi, tarehe ya kuchapishwa kitabu na namba ya kurasa ambayo umeipata hiyo taarifa. Kwa mfano: Katika kujaribu kuelewa maana ya Mwanzo 14:1-4, ni muhimu kutambua kwamba katika hadithi za Biblia “sehemu ambapo mjadala unatambulishwa kwa mara ya kwanza itakuwa ni sehemu muhimu katika kufunua tabia ya mzungumzaji. . .” (Kaiser na Silva 1994, 73). Hili bila shaka ni kweli kuhusu tabia ya Melkizedeki • Ukurasa wa “Kazi Zilizonukuliwa” mwishoni mwa chapisho au kazi yako ambao inatoa taarifa kuhusu vyanzo vya taarifa ulivyotumia.
EpukaWizi wa Kazi zaWatuWengine
Kutumia Nukuu za Marejeo
Kutumia Maelezo ya Nukuu Katika Kazi Yako
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker