Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
482 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
ambaye anatamka maneno ya baraka. Utambilisho huu wa Melkizedeki kama mamlaka chanya ya kiroho unaimarishwa na ukweli kwamba yeye ni Mfalme wa Salemu, kwani Salemu maana yake ni “salama, kwa amani” (Wiseman 1996, 1045).
Ukurasa wa “Kazi Zilizonukuliwa” unatakiwa kuwekwa mwishoni mwa kazi yako. Ukurasa huu: • Unaorodhesha kila chanzo ulichonukuu katika chapisho lako. • Unaandikwa katika mfumo wa kialfabeti kwa kuweka jina la mwisho la mwandishi • Unajumuisha tarehe ya uchapishaji na taarifa kuhusu mchapishaji. Kanuni zifuatazo za mpangilio zinapaswa kufuatwa: 1. Kichwa cha Habari Kichwa cha habari “Kazi Zilizonukuliwa” kinatakiwa kitumike na kuwekwa katikati katika mstari wa kwanza wa ukurasa baada ya mstari wa mpaka wa upande wa juu. 2. Maudhui Kila rejeo linatakiwa kuorodhesha: • Jina kamili la mwandishi (likianza na jina la mwisho) • Tarehe ya kuchapishwa • Kichwa cha habari na taarifa yoyote muhimu (toleo Jipya, toleo la pili, kuchapishwa upya) zilizochukuliwa kutoka kwenye jarada au ukurasa wa kichwa cha habari inatakiwa zionyeshwe. • Mji ambao mchapishaji ana makao yake makuu ikifuatiwa na nukta-mbili na jina la mchapishaji 3. Muundo wa Msingi • Kila taarifa inatakiwa itenganishwe kwa nukta. • Mstari wa pili wa marejeo (na mistari mingine yote inayofuata) inakiwa iwe imeingia ndani kidogo. • Vichwa vya habari vya kitabu vinatakiwa kupigiwa mistari (au kuandikwa kwa italiki). • Vichwa vya habari vya machapisho vinatakiwa viwekwe ndani ya fungua na funga semi.
Kutengeneza Ukurasa wa “Kazi Zilizonukuliwa”
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker