Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 489
Mchakato wa MAP Wanafunzi wa Stashahada
Kozi na mchakato wa MAP (Mpango wa Tathmini ya Huduma [Ministry Assessment Program] ) inalenga kuwawezesha wanafunzi kutafakari karama zao na wito wao katika huduma, na kuamua aina za mafunzo wanazohitaji kutafuta ili kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya uelekeo wa huduma zao zijazo. Tuna shauku ya kuwawezesha wanafunzi wetu wa TUMI kuhudumu vyema ndani ya makanisa yao, pamoja na viongozi wa madhehebu yao. Kwa mtazamo wetu, mafunzo ya hali ya juu ya huduma yanapaswa kuendana na wito na huduma ya mwanafunzi ndani ya maono ya huduma ya kusanyiko lake. Mchakato huo ni kama ufuatao: Itisha Mkutano wa Awali wa Kozi ya MAP • Itisha mkutano kwa ajili ya wale waliohitimu na wanaovutiwa na kozi ya MAP. • Chapisha Mpango wa Mafunzo ya Kozi (MMK) ya MAP kwa ajili ya kila mwanafunzi, pitieni pamoja mpango wa mafunzo, na kujibu maswali yoyote kuhusiana na kozi. Wanafunzi wote lazima wajinunulie vitabu vyao vya kiada. • Wape wanafunzi Mshauri wa Taaluma kwa ajili ya kozi hii (mapendekezo ya mwanafunzi yanapaswa kupewa uzito mkubwa katika uamuzi wa mwisho). • Tangaza tarehe ya mwisho kwa ajili ya kukusanya Insha ya Falsafa ya Huduma. Wasiliana na Mchungaji Msimamizi wa Mwanafunzi • Tuma barua kwa mchungaji wa mwanafunzi kwa niaba yake, pamoja na nakala kwa mwanafunzi. • Baada ya hapo mwanafunzi awasiliane na mchungaji wake, akimfahamisha kuhusu mahitaji ya kozi. Mchungaji akikubali kushiriki, basi itisha mkutano wa awali kwa ajili ya Mchungaji Msimamizi, Mshauri wa Taaluma, na mwanafunzi. • Mwanafunzi ataandika Insha ya Falsafa ya Huduma , akituma nakala kwa Mchungaji Msimamizi na Mshauri wake wa Taaluma.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker