Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

490 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

• Ratibu tarehe ya Mahojiano ya kwanza na Mwanafunzi, Mchungaji Msimamizi, na Mshauri wa Taaluma. Itisha Mkutano wa Kwanza na Mchungaji Msimamizi, Mwanafunzi, na Mshauri wa Taaluma • Mshauri wa Taaluma ataongoza mkutano huu, akiufuata Muhtasari wa Mahojiano ya Kwanza. • Mpe Mchungaji Msimamizi nakala ya MMK ya MAP. • Muelezee mwanafunzi na Mchungaji wake anayemsimamia hatua inayofuata: kukamilishwa kwa mpango wa huduma. Mwanafunzi na Mchungaji Msimamizi wanapaswa kujadili mara kwa mara maendeleo ya kazi hii ili kukamilisha maelezo ya kazi. • Panga tarehe kusudiwa kwa ajili ya kukamilisha Mpango wa Huduma, yaani, utakapo wasilishwa kwa Mshauri wa Taaluma na kwa Mchungaji Msimamizi. • Panga tarehe (makisio) kwa ajili ya mkutano ujao na Mchungaji Msimamizi na Mwanafunzi. Itisha Mkutano wa Pili na Mchungaji Msimamizi, Mwanafunzi, na Mshauri wa Taaluma • Mshauri wa Taaluma ataongoza mkutano huu akiufuata Muhtasari wa Mahojiano ya Mwisho. • Kusanya Kazi za Usomaji za mwanafunzi. • Kusanya Kazi ya Mwanafunzi ya Utetezi wa Kanuni ya Imani ya Nikea. • Saini karatasi ya Makubaliano ya Mpango wa Huduma Chini ya Usimamizi (Mwanafunzi, Mchungaji Msimamizi, na Mshauri wa Taaluma) na kuiambatanisha na nakala ya mpango wa huduma ya Mshauri wa Taaluma. • Panga tarehe ya kukutana na mwanafunzi ili kunukuu mbele ya Mshauri wa Taaluma Kanuni ya Imani ya Nikea (neno kwa neno). • Panga tarehe (makisio) kwa ajili ya Mwanafunzi kukutana na Mchungaji Msimamizi ili kupitia Maswali kwa ajili ya Mikutano ya Huduma Chini ya Usimamizi.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker