Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
492 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Mpango wa Mafunzo ya Kozi C3-303 Kazi ya Tathmini ya Huduma
Credit Hours: 3 credits Idara: Huduma ya Kikristo
I. Maelezo na Malengo ya Kozi Kozi hii imeundwa ili kuwasaidia wanafunzi kutafakari juu ya karama zao na wito wao katika huduma, ili kuwasaidia kuamua aina za mafunzo wanazohitaji kutafuta ili kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya uelekeo wa huduma zao zijazo, na kuwasaidia wanafunzi kufanya kazi na viongozi wao wa makanisa au madhehebu ili kuhakikisha kwamba mafunzo haya yanaunganishwa na maono ya huduma ya jumuiya zao. Baada ya kuchukua kozi hii, kila mwanafunzi anapaswa kuwa na uwezo wa: • Kuelezea bayana wito wake wa huduma na maono yake kwa ajili ya huduma ya baadaye. • Kutambua kanuni za msingi za kitheolojia za kanisa, huduma na uongozi ambazo zitaongoza maendeleo yake katika huduma. • Kuelezea jinsi karama zake za kiroho zinavyoweza kuboresha huduma yake. • Kutambua maeneo ambayo watahitaji kutafuta mafunzo zaidi na kuyatumia katika kama msingi wa elimu yao katika ngazi ya Stashahada ya Masomo ya Huduma. • Kutengeneza mpango utakaoidhinishwa na mamlaka ya kichungaji kwa ajili ya mafunzo ya huduma kwa vitendo chini ya uangalizi ndani ya kusanyiko au dhehebu lake. II. Vitabu na Nyenzo Cothen, Joe H. and Jerry N. Barlow. Equipped for Good Work: A Guide for Pastors . Rev. ed. Gretna, LA: Pelican Publishing, 2002. Sanders, J. Oswald. Spiritual Leadership: Principles of Excellence for Every Believer . Rev. ed. Chicago: Moody Press, 1984. Schmitt, Harley H. Many Gifts, One Lord . Fairfax, VA: Xulon Press, 2002.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker