Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 493

III. Mahitaji ya Kozi Muhtasari wa Mfumo wa Kutunuku Matokeo na Uzito wa Gredi 1) Mikutano na Mshauri . . . . . . . . . 10% 2) Muhtasari wa Usomaji . . . . . . . . . 15% 3) Insha ya Falsafa ya Huduma 20% 4) Mapitio ya Muhtasari wa Fundisho . . . . 20% 5) Kazi ya Kukariri Kanuni ya Imani ya Nikea 20% 6) Mpango wa Huduma (ashirikishwe kiongozi wa huduma au mchungaji msimamizi) 15% 100 pts Mambo ya Kuzingatia katika Utoaji Maksi Mikutano ya Awali na Mshauri wako Utahitajika kukutana na mshauri wako wa kitivo ili kujadili kazi mbalimbali utakazohitaji kukamilisha ili kukamilisha kozi ya MAP. Kazi hizi zitajumuisha kukamilisha kwako muhtasari wa Usomaji, Insha yako ya Falsafa ya Huduma, Mapitio ya Muhtasari wa fundisho, Kazi ya Kukariri Kanuni ya Imani ya Nikea, na uundaji wa Mpango wa Huduma ambao utamshirikisha kiongozi wako wa huduma au mchungaji msimamizi. Nia yetu ni kwamba umshirikishe kiongozi wako kuhsu mpango wako wa hatua inayofuata ya huduma. Kuhusu Mchungaji msimamizi wako, huyu atakuwa mchungaji wako kiongozi au kiongozi aliyeteuliwa na mchungaji wako kiongozi. Ikiwa wewe ni mchungaji kiongozi, unaweza kuchagua mojawapo kati ya wafuatao: a) msimamizi wa dhehebu, [k.m. Askofu, Mwangalizi, n.k], au b) mchungaji mwingine kutoka katika jamii yako anayeaminika, ambaye ana uzoefu zaidi yako na ambaye yuko tayari kuwekeza katika maendeleo yako ya huduma. Muhtasari wa Usomaji (Taz. Kiambatisho cha Kwanza) Usomaji na “ripoti za usomaji” vimeundwa ili kukusaidia kuchagua kanuni muhimu za huduma kutoka kwenye kila usomaji na kuzitumia kwenye hali yako ya huduma. Haya yanatakiwa kukusanywa siku ya mkutano wa mwisho na mshauri wako wa taaluma na mchungaji msimamizi. Insha ya Falsafa ya Huduma (Taz. Kiambatisho cha Pili) Insha ya Falsafa ya Huduma inakupa fursa ya kutafakari juu ya wito wako wa huduma, uzoefu wako wa huduma, karama zako za rohoni, malengo yako ya baadaye, na maeneo ambayo unaweza kuhitaji mafunzo na uwekezaji zaidi.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker