Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

494 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Mapitio ya Muhtasari wa Fundisho Ili kuwa mhudumu bora wa Injili, lazima uweze kutetea kanuni kuu za imani ya kitume zilizofupishwa katika mada za theolojia ya utaratibu. Utahitaji kuandika aya moja kwa kila mojawapo ya mafundisho muhimu yafuatayo ya imani ya Kikristo: fundisho la Neno la Mungu, fundisho la Mungu (ikiwemo na mada ya Utatu), fundisho la Kristo, fundisho la Roho Mtakatifu, fundisho la malaika, fundisho la wokovu, fundisho la kanisa, fundisho la Ufalme, na fundisho la mambo ya mwisho. Hii haikusudiwi kuwa risala nzito ya kitheolojia; unatakiwa tu kuandika uelewa wako bora zaidi wa mawazo muhimu na ukweli unaohusishwa na kila mada. Nukuu Maandiko inapohitajika, na zingatia mafundisho makuu ya kila kichwa. Kazi ya Kukariri Kanuni ya Imani ya Nikea (Taz. Kiambatisho cha Tatu) Ili kutimiza mahitaji ya kozi ya MAP, utahitaji kuandika (au kunukuu) Kanuni ya Imani ya Nikea kifungu-kwa-kifungu, pamoja na marejeo ya Biblia yanayoambana na kila kifungu. Utahitaji pia kukariri mistari ya Maandiko ambayo imeorodheshwa katika safu ya kulia inayowakilisha vifungu muhimu kwa kila kifungu. Pengine Kanuni ya Imani ya Nikea ndiyo tamko muhimu zaidi la kitheolojia katika historia ya Kanisa, na inawakilisha muhtasari mfupi na wa wenye nguvu wa fundisho la kitume. Ikiwa imeandikwa katika karne ya 4, imestahimili kipimo cha wakati, ikitumika kama msingi wa uthibitisho wa imani, kuweka wakfu watumishi na kwa ajili ya huduma ya Injili. Tafadhali jiwekee lengo la kukariri Kanuni ya Imani ya Nikea neno kwa neno na vifungu vya rejea neno kwa neno. Ili kufaulu kozi hii, haupaswi kufanya jumla ya makosa zaidi ya kumi. Mpango wa Huduma na Majadiliano na Mchungaji Msimamizi (Taz. Kiambatisho cha Nne) Hitaji lako la mwisho la kozi linahusisha rasimu yako ya mpango wa huduma ambayo utaiandaa, na kuipitia pamoja na kiongozi wako wa huduma au mchungaji msimamizi wako. Lengo la mazungumzo haya ni kupata ushauri, mchango, na tathmini ya matamanio yako ya baadaye ya huduma ili uweze kugundua fursa mpya na changamoto kwa huduma yako endelevu inayokua. Baada ya mazungumzo yako na mchungaji msimamizi, lazima uwasilishe kwa mchungaji msimamizi na mshauri wako nakala za mpango wako uliokamilika.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker