Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 495

Kiambatisho cha Kwanza: Muhtasari wa Usomaji

1. Theolojia ya Uongozi Soma Spiritual Leadership: Principles of Excellence for Every Believer cha J. Oswald Sanders na kisha: a. Jibu maswali ya kujifunzia yaliyo mwishoni mwa kitabu kwenye ukurasa wa 167-179. (Hili linaweza kufanywa baada ya kila sura kwa ajili ya ufanisi mkubwa zaidi). b. Baada ya kumaliza maswali haya ya kujifunzia, tafadhali jibu maswali yafuatayo pia, “Ni ufahamu gani muhimu zaidi uliopata kutoka kwenye kitabu?” na “Je! Unataka hilo liathiri vipi namna unavyohudumia wengine?” 2. Theolojia ya Huduma Soma Equipped for Good Work: A Guide for Pastors cha Joe H. Cothen na Jerry N. Barlow na kisha andika andiko fupi lenye majibu ya maswali yafuatayo: a. Je! Ufafanuzi upi unaelezea kwa ubora zaidi kusudi la huduma ya kichungaji? (Tetea jibu lako). b. Chagua kipengele kimojawapo kati ya vipengele vifuatavyo vya huduma ya kichungaji (kuhubiri na kufundisha, uinjilisti, uongozi wa ibada, ubatizo na Meza ya Bwana, au msaidizi wa wagonjwa, wanaoumia na waliofiwa) na ueleze ni upi ulio wajibu muhimu zaidi wa mchungaji katika eneo hili na ni maandalizi gani yanahitajika ili kuufanya vizuri. c. “Ni ufahamu gani muhimu zaidi uliopata kutoka kitika kitabu?” d. “Kama kiongozi wa Kikristo uliyeitwa katika huduma ya kichungaji, unataka ukweli wa kitabu hiki uathiri vipi namna unavyohudumia wengine?” AU “Kama kiongozi wa Kikristo ambaye hujaitwa katika huduma ya kichungaji, ni njia zipi ambazo maarifa kutoka katika kitabu hiki yanapaswa kuathiri jinsi unavyohudumia wengine?”

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker