Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

496 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

3. Theolojia ya Karama za Rohoni Soma Many Gifts, One Lord cha Harley H. Schmitt na kisha andika aniko fupi linalojibu maswali yafuatayo:

a. Kwa uelewa wako wa “karama za rohoni” neno hilo lina maana gani? (Tumia Maandiko kuunga mkono ufafanuzi wako). b. Kuna uhusiano gani kati ya “karama za rohoni” na “neema ya Mungu?” c. Kuna uhusiano gani kati ya “tunda la Roho” na “karama za Roho?” d. Je, kuna maeneo ya kutokubaliana ambayo wewe (au kanisa lako) linaweza kuwa nayo kwa kuzingatia namna Mchungaji Schmitt anavyoelewa karama za rohoni na matumizi yake? Ikiwa yapo, ni yapi na unawezaje kufafanua na kutetea tofauti hizo? e. Je, unatumia karama zipi za rohoni katika huduma yako? Umegunduaje karama hizi? f. Je, katika uhalisia unahudumu kwenye maeneo ya karama yako? Ikiwa ndivyo, unajuaje? Ikiwa sivyo, unawezaje kuchukua hatua kuelekea kufanya hivyo? g. Unahakikishaje kwamba karama zako zinatumika kwa ajili ya kuhudumia kusanyiko lako badala ya kutumika tu kama namna ya kumtosheleza mtu binafsi? h. “Ni ufahamu gani muhimu zaidi ulioupata kutoka katika kitabu?” na “ungetamani ufahamu huu uathiri kwa namna gani njia unazotumia kuwahudumia wengine?”

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker