Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 497

Kiambatisho cha Pili: Insha ya Falsafa ya Huduma Andika insha ambayo inakusaidia kuweka wazi kwako na kwa wengine wito wako wa huduma na njia ambazo umejiandaa au utajiandaa kutimiza wito wako. Ili kukusaidia kufanya hili, tunakuomba uandike insha hii kwa kujibu mfululizo wa maswali yafuatayo: Sehemu ya Kwanza: Wito 1. Mungu alikuitaje katika huduma yako ya sasa?* a. Majukumu yako ya sasa kwenye huduma ni yapi? b. Je, kuna watu au matukio yoyote ambayo Mungu kipekee kabisa alitumia kukuongoza katika huduma hii? c. Je, kuna mstari maalum wa Maandiko au kifungu ambacho Mungu alitumia kukuongoza kwenye huduma? d. Uongozi wa kichungaji wa kanisa lako umethibitishaje wito wako? 2. Je, unaweza kufafanuaje wito ulio kwenye maisha yako? a. Je, Mungu ameweka mizigo, shauku, na matamanio gani moyoni mwako kama kiongozi? b. Ni karama gani za kiroho unazotumia katika huduma yako na umegunduaje karama hizi? c. Ni kwa namna gani wito wako umekuwa ukidhihirishwa wazi zaidi kadri muda unavyosonga? d. Kwa sasa unaishije wito huu? e. Kuuishi wito wako kumeleta imani na misimamo gani katika maisha yako? f. Iwapo ungetakiwa kufafanua katika sentensi moja tu kile ambacho umeitwa kufanya, ungesemaje? 3. Una maono gani ya baadaye kwa ajili ya huduma? a. Je, una ndoto gani kuhusu namna ambayo ungependa kuona Mungu akikutumia siku za usoni? b. Ni vizuizi gani vinasimama kati yako na kuishi kwako kikamilifu wito wako? c. Ni aina gani za huduma umeweza kuzifanya kwa matokeo au ufanisi hadi sasa na hilo linaashiria nini kuhusu uelekeo wa huduma yako katika siku zijazo?

* Tunaposema huduma, hatumaanishi huduma ya kichungaji pekee. Ikiwa Mungu amekuita kwenye uongozi unaotambulika

katika eneo lolote la maisha ya kanisa au uenezi iwe wa walei au wa kichungaji, tunaamini mchakato huu wa tathmini utakuwa wa thamani kwako na kwa kanisa lako.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker