Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

498 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

d. Utahakikishaje kwamba maendeleo yako ya huduma yamejengwa imara katika kusanyiko lako la kanisa,

yanaungwa mkono na viongozi wa kanisa lako, na yanaweka mahitaji ya jumuiya ya kanisa juu ya mahitaji yako binafsi?

Sehemu ya Pili: Maandalizi 4. Mungu amekwisha kukuandaa kwa namna gani ili kutimiza wito wako? a. Ni watu gani, uzoefu, na/au mafunzo rasmi ambayo yamekutayarisha kwa ajili ya huduma hadi sasa? b. Je, ni mambo gani muhimu umejifunza kupitia mambo yaliyojadiliwa hapo juu? 5. Je, ni uzoefu gani wa maisha na kozi za mafunzo ambazo utahitaji ili kutimiza maono yako ya baadaye kwa ajili ya huduma? a. Ni “mapengo” gani yaliyopo katika maandalizi yako ya huduma? b. Ni mambo gani unayotaka kujifunza zaidi ili kujiandaa vyema? c. Ni kozi gani za TUMI ambazo ungehitaji kuchukua zaidi? d. Ni kozi gani mpya ambazo ungetamani TUMI itoe kazika vipindi vijavyo? e. Ni masomo gani ya kujitegemea na/au mafunzo ya huduma chini ya usimamizi yanaweza kusaidia? f. Je, ni fursa gani ungependa kuchunguza pamoja na mchungaji wako ili kuona jinsi kanisa lako au uongozi wa dhehebu lako unavyoweza kuwekeza katika maandalizi yako ya uongozi?

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker