Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 499

Kiambatisho cha Tatu: Kanuni ya Imani ya Nikea

Tuna amini katika Mungu mmoja, (Kum. 6:4-5; Marko 12:29; 1 Kor. 8:6) Baba Mwenyezi, (Mwa. 17:1; Dan. 4:35; Mt. 6:9; Efe. 4:6; Ufu. 1:8) Muumba wa mbingu na nchi (Mwa 1:1; Isa. 40:28; Ufu. 10:6) Na vitu vyote vinavyoonekana na visivyo onekana (Zab. 148; Rum. 11:36; Ufu. 4:11) Tuna amini katika Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana pekee atokaye kwa Mungu, Aliyezaliwa na Baba kabla ya nyakati zote, Mungu atokaye kwa Mungu, nuru itokayo katika nuru, Mungu wa kweli atokaye kwa Mungu wa kweli. Aliyezaliwa na si kuumbwa, Mwenye asili moja na Baba, (Yoh. 1:1-2; 3:18; 8:58; 14:9-10; 20:28; Kol. 1:15, 17; Ebr. 1:3-6) Katika yeye vitu vyote vilifanyika (Yohana 1:3; Kol. 1:16) Ambaye kwa ajili yetu na kwa ajili ya wokovu wetu alishuka kutoka mbinguni na alifanyika mwili kwa Roho Mtakatifu na bikira Mariamu na kuwa Mwanadamu. (Mt. 1:20-23; Yohana 1:14; 6:38; Luka 19:10) Ambaye kwa ajili yetu pia alisulibiwa chini ya Pontio Pilato, akateseka na akazikwa. (Mt. 27:1-2; Marko 15:24-39, 43-47; Mdo 13:29; Rum. 5:8; Ebr. 2:10; 13:12) Siku ya tatu akafufuka kama yasemavyo Maandiko. (Marko 16:5-7; Luka 24:6-8; Mdo 1:3; Rum 6:9; 10:9; 2 Tim. 2:8) Akapaa mbinguni, na ameketi mkono wa kuume wa Baba. (Marko 16:19; Efe. 1:19-20) Atarudi tena katika utukufu, kuhukumu walio hai na wafu, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. (Isa. 9:7; M,t. 24:30; Yohana 5:22; Mdo 1:11; 17:31; Rum. 14:9; 2 Kor. 5:10; 2 Tim. 4:1) Tuna amini katika Roho Mtakatifu, aliye Bwana na Mpaji wa uzima, (Mwa. 1:1-2; Ayu 33:4; Zab. 104:30; 139:7-8; Luka 4:18-19; Yohana 3:5-6; 1:1-2; 1 Kor. 2:11; Ufu. 3:22) Ambaye anatoka kwa Baba na kwa Mwana, (Yohana 14:16-18, 26; 15:26; 20:22) Ambaye pamoja na Baba, na Mwana, anaabudiwa na kutukuzwa. (Isa. 6:3; Mt. 28:19; 2 Kor. 13:14; Ufu. 4:8) Ambaye alinena kupitia manabii. (Hes. 11:29; Mik. 3:8; Mdo 2:17-18; 2 Pet. 1:21)

Tunaamini katika Kanisa moja takatifu, Katoliki na la Kitume. (Mt. 16:18; Efe. 5:25-28; 1 Kor. 1:2; 10:17; 1 Tim. 3:15; Ufu. 7:9)

Tunatambua ubatizo mmoja kwa ajili ya msamaha wa dhambi, (Mdo 22:16; 1 Pet. 3:21; Efe. 4:4-5) Na tunatazamia kufufuliwa kwa wafu na maisha ya wakati ujao (Isa. 11:6-10; Mik. 4:1-7; Luka 18:29-30; Ufu. 21:1-5; 21:22-22:5). Amen.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker