Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 501

Kiambatisho cha Nne: Mpango wa Huduma Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.

~ Mit. 16:9 (SUV)

Kulingana na maarifa uliyopata kupitia usomaji wako, Insha ya Falsafa ya Huduma na Mapitio ya Muhtasari wa Fundisho, na mkutano wako wa awali na msimamizi wako, utahitajika kuandaa mpango ambao unatoa muhtasari wa matamanio yako ya baadaye ya huduma. Maswali haya yameundwa ili kukusaidia kuelewa na kueleza, kadiri uwezavyo, hatua zinazofuata katika maandalizi yako ya huduma, katika eneo unaloamini kwamba Mungu amekuita kutumika. Jibu maswali yafuatayo kwa uaminifu kadiri iwezekanavyo, na uwe tayari kuwashirikisha hoja za majibu yako mchungaji msimamizi na mshauri wako. 1. Malengo Yangu ya Huduma ni Yapi? a. Andika kauli ya maono (dira) ambayo inaelezea kile unachotaka kutimiza katika huduma. George Barna anasema kwamba“Maono kwa ajili ya huduma ni taswira ya kile ambacho Mungu anataka kutimiza kupitia wewe ili kujenga Ufalme wake” na anafafanua kauli za maono kama “picha ya wakati ujao iliyo bora zaidi na ya wazi akilini ambayo Mungu amewapa watumishi wake wateule” yaani “iliyojengwa katika ufahamu sahihi wa Mungu, wa mtu, na wa mazingira.”* Kwa hivyo, tamko na kauli yako ya maono inapaswa kusema wazi na kwa ufupi kile unachotaka kufanya na kutimiza katika huduma. Kauli hii inapaswa kuchukua kwa uzito kile ambacho unaamini kwamba Mungu ameweka ndani ya moyo wako na pia mchango wa mawazo kutoka kwa mchungaji wako msimamizi. b. Kwa kutumia maarifa uliyopata katika insha yako ya Falsafa ya Huduma, andika: • Angalau malengo matatu ya muda mfupi ya huduma (mambo ambayo utajaribu kukamilisha katika kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja) • Angalau malengo matatu ya muda mrefu ya huduma (mambo ambayo utajaribu kutimiza katika miaka miwili hadi mitano ijayo). Malengo haya yanapaswa kukusaidia kufanya maendeleo kuelekea yale uliyoandika katika taarifa yako ya maono. Yanaweza kujumuisha vyote viwili: • Malengo ya maendeleo ya kiroho (njia ambazo unataka kukua katika nidhamu za kiroho [maombi, kufunga, kusoma Maandiko na kuyakariri, n.k.] au njia ambazo unataka kukua katika ukomavu wa kiroho).

* George Barna, The Power of Vision: How You Can Capture and Apply God’s Vision for Your Ministry , (Ventura, CA: Regal

Books, 1992), kurasa 28-29.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker