Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
502 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
• Malengo ya stadi za huduma (njia ambazo unataka kuongeza uzoefu wako na umahiri katika kufanya kazi za huduma). Kumbuka: Malengo mazuri yanakuwa na sifa zifuatazo: • Mahususi (ikiwezekana tabia zinazoonekana) • Yanayoweza kupimika (ngapi, kwa muda gani) • Yanayoweza kufikiwa (kwa rasilimali zilizopo) • Halisi (kwa lengo la wito wako au ukuaji binafsi) • Yanayofuata wakati (ndani ya muda gani hasa)* 2. Ni Kazi Gani ya Kozi za Theolojia na Huduma Ninayopaswa Kuzingatia Zaidi? Kwa kutumia maarifa uliyopata katika insha yako ya Falsafa ya Huduma, andika aina za kozi ambazo ungependa zaidi kuchukua ili kutimiza malengo yako ya huduma ya muda mfupi na ya muda mrefu. 3. Je, Ninawezaje Kuwa Mahiri katika Ufahamu wa Sifa Maalum Dhehebu (au Kikusanyiko) Langu? Kozi za kitheolojia za TUMI zimeundwa ili kukusaidia kuelewa na kutetea mafundisho makuu ya imani ya Kikristo kama yanavyoelezwa kwa ufupi katika Kanuni ya Imani ya Nikea. Mafunzo haya yanakazia kile ambacho Wakristo wote wanaamini kwa pamoja katika uelewa wao wa imani. Hata hivyo, huduma yako itatokea kama sehemu ya dhehebu (au kusanyiko linalojitegemea) ambalo lina sifa maalum za kifundisho na desturi za huduma zinazotofautisha kanisa lako na vikundi vingine vya Kikristo. Unahitaji kutengeneza mpango wa kusoma au njia nyingine ambayo itakusaidia kujifunza mafundisho na desturi maalum za kusanyiko lako na kanuni za Kimaandiko zinazoyaunga mkono. 4. Ni Huduma Ipi Nitakayotekeleza Chini ya Uangalizi? a. Ni huduma gani nitakayofanya chini ya uangalizi kwa niaba ya kanisa langu? b. Huduma hii chini ya usimamizi itadumu kwa muda gani? c. Je, mchungaji wangu anayenisimamia atatoa usimamizi wa moja kwa moja kwa huduma hii au kutakuwa na mtu mwingine atakayepewa jukumu la kusimamia maendeleo yangu? d. Ni mara ngapi nitakutana na mchungaji msimamizi au mtu atakayeteuliwa kunisimamia? e. Nyakati hizi za kukutana kwetu zitahusisha nini? (Taz. Kiambatisho cha Tano) f. Nitaonyeshaje kwamba ninatumia kanuni nilizojifunza kutoka kwenye kazi za usomaji katika huduma yangu?
* Imechukuliwa kutoka kwa Gary
Pearson, “Designing a Learning Covenant,” in Experiencing Ministry Supervision , William T. Pyle and Mary Alice Seals, wah., (Nashville: Broadman and Holman Publishers, 1995), uk. 60
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker