Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 503

Kiambatisho cha Tano: Maswali kwa ajili ya Mikutano ya Huduma chini ya Usimamizi Maswali yafuatayo yanatolewa kama kichocheo cha kuhimiza mawasiliano ya wazi na ya uaminifu kati yako kama mchungaji msimamizi na mwanafunzi wa TUMI. Ili kutimiza mahitaji ya kozi yetu ya Kazi ya Tathmini ya Huduma, mwanafunzi ana jukumu la kujadiliana na wewe kuhusu changamoto na fursa zinazohusiana na huduma yake katika nafasi yake ya sasa kanisani, pamoja na malengo yake ya baadaye ya huduma. Tunatoa maswali haya ili kukusaidia katika kumsaidia mwanafunzi kuelewa karama zake, fursa, na wito wake anapofikiria huduma yake ya baadaye katika kanisa. Kumbuka: Tafadhali jisikie huru kuandika maswali yako mwenyewe unapojadiliana na mwanafunzi kuhusu kufaa kwake na kupatikana kwake kwa ajili ya huduma. 1. Je, kwa sasa unatoa muda gani kwa eneo hili la huduma – kila wiki, kila mwezi, n.k.? Ni kiasi gani cha muda huo kinatumika kwa ajili ya maandalizi na ni kiasi gani kinatumika katika huduma ya moja kwa moja? 2. Una majukumu na wajibu gani wa huduma sasa kuhusiana na nafasi hiyo? 3. Je, una hisia gani na mwitikio upi kwa sasa kwa habari ya eneo hili la huduma? Je, kuna maeneo yoyote ya kukatisha tamaa au kufadhaisha? Je, kuna migogoro yoyote inayohitaji kutatuliwa? Elezea. 4. Wale wanaohudumiwa wanaitikiaje jitihada na utumishi wako pamoja na wengine katika eneo hili la utumishi? Eleza. 5. Je, wewe na wafanyakazi wenzako mnaelewana na mnahusiana vipi katika nafasi yako ya sasa? Je, ni maarifa gani kuhusu uongozi na utendaji katika timu ambayo unayapokea kutokana na uzoefu huo? 6. Je, unaweza kusema una changamoto gani tatu kuu kwa wakati huu katika huduma hiyo? 7. Ni jambo gani la maana zaidi au la kutia moyo ambalo limetukia kupitia huduma yako tangu tulipozungumza mara ya mwisho? 8. Je, unaweza kueleza nini kuhusu mambo matatu muhimu zaidi uliyojifunza tangu tulipokutana mara ya mwisho kujadili kuhusu huduma yako ya sasa? 9. Je, eneo hili la huduma na uenezi linaendana vyema na karama na ujuzi wako wa huduma? Ikiwa ndio, kwa jinsi gani? Ikiwa sivyo, kwa nini?

Tafadhali mpe fomu hii kiongozi wa huduma yako au mchungaji anayekusimamia.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker