Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
508 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
7. Alika Mchungaji Msimamizi, mwanafunzi, na wewe mwenyewe kutia sahihi nakala ya “Mkataba wa Mpango wa Huduma chini ya Usimamizi” na uiambatanishe na nakala ya Mpango wa Huduma ya Mshauri wa Taaluma. (Ikiwa mpango unahitaji kurekebishwa kwa kuzingatia maswali yaliyoulizwa wakati wa mahojiano, chagua kisanduku kinachofaa kwenye fomu na uambatanishe na nakala iliyorekebishwa itakapokuwa tayari). 8. Kusanya Ripoti za Usomaji za mwanafunzi na Andiko lake la Utetezi wa Kanuni ya Imani ya Nikea. 9. Panga tarehe ya kukutana na mwanafunzi kwa ajili ya kunukuu Kanuni ya Imani ya Nikea mbele ya Mshauri wa Kitaaluma (neno-kwa-neno). 10. Panga tarehe ya makisio kwa ajili ya Mwanafunzi kukutana na Mchungaji Msimamizi ili kupitia Maswali ya Mikutano ya Huduma Inayosimamiwa. 11. Hitimisha kwa muda mfupi wa maombi. Mshukuru Mchungaji Msimamizi na mwanafunzi, na uwatie moyo kuhusu jinsi Mungu anavyowatumia kujenga Ufalme wake.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker