Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 507

Mwongozo kwa ajili ya Mahojiano ya Mwisho Na Mshauri wa Taaluma, Mwanafunzi, na Mchungaji Msimamizi

1. Wakaribishe mwanafunzi na Mchungaji Msimamizi na uwashukuru kwa kuja. 2. Mkumbushe mwanafunzi kuwa uzoefu bila kutafakari sio elimu. Hakikisha anaelewa kwamba wanapaswa kutumia ripoti za usomaji na mikutano pamoja na mchungaji anayemsimamia kutafakari juu ya uzoefu wa huduma alio nao na ili kuboresha namna yake ya kufanya kazi za huduma. 3. Muulize Mchungaji Msimamizi kama wamesoma mpango wa huduma na kama ana maswali yoyote kuuhusu. 4. Muulize mwanafunzi kama kuna swali lolote akilini mwake kuhusu sehemu yoyote ya mpango ambao ameupendekeza, hasa kuhusu maelezo ya kazi ya huduma inayosimamiwa na usimamizi wake. 5. Mwambie mwanafunzi afanye muhtasari wa mambo muhimu zaidi aliyojifunza kutokana na mchakato huu. Panua mjadala kwa kuuliza maswali yafuatayo: a. Je, wito wako umebadilishwa, kufafanuliwa au kuthibitishwa vipi? b. Je, kuna mambo yoyote ambayo ungebadilisha katika Andiko lako la Falsafa ya Huduma au Mpango wa Huduma ikiwa ungeyaandika upya baada ya kupata uzoefu huu? c. Je, usomaji ulichangia nini katika uelewa wako wa huduma? d. Je, una malengo mapya ya muda mfupi au mrefu kwa kuzingatia yale uliyojifunza? 6. Muulize Mchungaji Msimamizi kile alichojifunza kuhusu mwanafunzi na kile anachoamini Mungu anaweza kusema au kufanya katika maisha na wito wa huduma ya mwanafunzi. Je, kuna hatua zozote zinazofuata ambazo Mchungaji Msimamizi angependa kupendekeza kwa mwanafunzi?

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker