Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
506 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
7. Mwulize Mchungaji Msimamizi kama kuna njia zozote ambazo angependekeza kwa mwanafunzi kupata ufahamu wa kina wa sifa maalum za dhehebu au za kusanyiko lao. 8. Hitimisha mkutano kwa maagizo na vikumbusho vifuatavyo: a. Hatua inayofuata kwa mwanafunzi ni kukamilisha mpango wa huduma. Weka tarehe inayopendekezwa ya kukamilisha kazi hiyo. Kazia kwa mwanafunzi kwamba itabidi akutane na kuzungumza na mchungaji msimamizi wake wakati mpango wa hudu ukiandaliwa ili kukamilisha mambo yote yahusuyo mafunzo husika ya huduma. b. Panga tarehe ya makisio kwa ajili mkutano wa pili. Mkumbushe mwanafunzi kwamba atapaswa kutuma nakala za mpango wa huduma Mshauri wa Taluma na Mchungaji Msimamizi kabla ya mkutano unaofuata. c. Mkumbushe mwanafunzi kwamba atahitaji kuwasilisha Ripoti zake za Usomaji na Andiko lake la Utetezi wa Kanuni ya Imani ya Nikea katika mkutano wenu unaofuata. d. Muulize mwanafunzi na msimamizi kama wana maswali yoyote zaidi. e. Funga kwa kumuombea mwanafunzi na Mchungaji Msimamizi.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker