Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
MPANGO WA TATHMI N I YA HUDUMA / 505
Mwongozo kwa ajili ya Mahojiano ya Kwanza Na Mshauri wa Taaluma, Mwanafunzi, na Mchungaji Msimamizi
1. Mkaribishe Mchungaji Msimamizi na mwanafunzi na uwatie moyo na kuwaonyesha matarajio kuhusu thamani ya mchakato huu. Eleza hukusu Stashahada ya Mafunzo ya Huduma na sisitiza kwamba muundo wake unatoa jukumu kuu la mafunzo kupitia wachungaji wa kanisa la mahali pamoja. Mpe Mchungaji Msimamizi nakala ya Mpango wa Mafunzo ya Kozi . (Kumbuka: Mkumbushe mwanafunzi kuandika madokezo juu ya kila kitu ambacho Mchungaji Msimamizi anaeleza kwa sababu yanapaswa kutiliwa maanani katika kuunda mpango wao wa huduma). 2. Mwombe mwanafunzi azungumze kwa ufupi jinsi anavyoweza kufafanua malengo yake ya muda mrefu katika huduma na ni aina gani za mafunzo anazohisi anahitaji ili kufikia malengo hayo. 3. Muulize Mchungaji Msimamizi kama ana maoni yoyote kuhusu Andiko la Falsafa ya Huduma ya mwanafunzi. Baada ya maoni haya kutolewa na kujadiliwa, mwambie msimamizi afafanue ni aina gani ya majukumu ya uongozi anayotarajia kumpa mwanafunzi na ni aina gani ya huduma ambayo angependa kuona anahusika nayo. 4. Waombe mwanafunzi na Mchungaji Msimamizi kwa pamoja wapate kutafakari juu ya karama za rohoni wanazoamini kwamba mwanafunzi anazitumia kanisani. 5. Mwombe mwanafunzi azungumzie aina ya huduma ambayo angependa kuhusika nayo chini ya usimamizi na jinsi inavyoweza kuonekana. 6. Mwambie Mchungaji Msimamizi aongee kuhusu aina ya shughuli za huduma ambamo anaweza kumweka mwanafunzi ambazo zinaweza kumnufaisha mwanafunzi na kanisa pia. (Mpe Mchungaji Msimamizi nakala ya kitini cha aina za usimamizi na upendekeze kwamba akitumie kama nyenzo anapozungumza na mwanafunzi kuhusu jinsi shughuli ya huduma itakavyosimamiwa. Sisitiza kwamba jukumu la kuamua namna usimamizi liko juu yake kabisa na kwamba kitini hicho ni kwa madhumuni ya kuchochea mawazo tu).
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker