Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

UTANGUL I Z I WA FUNGU LA MASOMO YA B I B L I A / 81

huduma ya Yesu. Kwa kufanya hivyo, utaweza kuwa mfuasi wake na kufanya wanafunzi wa Yesu katika kanisa lako, katika huduma yako, na popote pengine ambapo Mungu anaweza kukuongoza. Jitwike nira yake, na ujifunze kwake – huu ndio ufunguo wa uongozi wa mtumishi wa Mungu katika Kristo. Ombi langu la dhati ni kwamba baraka hizi zote na zaidi ziwe juu yako kadiri Roho Mtakatifu anavyokuwezesha kuchunguza kanuni na mbinu za kufasiri Neno lake takatifu na la milele!

Kazi za Fungu Hili Kama sehemu ya ushiriki wako katika Mtaala wa Cornerstone, utahitajika kufanya ufafanuzi, yaani eksejesia (uchambuzi wa ndani wa andiko) kuhusu kifungu kimojawapo cha Neno la Mungu:

Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko

a. Zaburi 110:1-4 b. Isaya 55:1-10 c. Luka 24:36-48 d. 2 Timotheo 3:14-17

Kusudi la kazi hii ya ufafanuzi wa Maandiko ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu mojawapo mihimu kuhusu asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya vifungu vilivyopo hapo juu (au andiko ambalo wewe na mkufunzi wako mtakubaliana ambalo huenda halipo kwenye orodha), tunatumai kwamba utaweza kuonyesha jinsi kifungu hiki kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa hali yetu ya kiroho na kwa maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe utambuzi wa jinsi unavyoweza kuhusianisha maana ya kifungu husika moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi wako, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika maudhui yake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa kutamka au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. a. 2 Timotheo 3:16-17 b. Zaburi 1.1-3 c. Luka 24:44-48 d. Yohana 15:18-20

Kukariri Maandiko

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker