Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

80 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

na litahakikisha mtu wa Mungu anafurahia mafanikio mema katika yote anayofanya ili kuendeleza Ufalme wa Mungu popote alipo (Yoh. 10:35; Isa. 55:8-11; Yos. 1:8). Maandiko yenye pumzi ya Roho yamejengwa juu ya ushuhuda wa Yesu wa Nazareti. Yeye pekee ndiye anayetoa umoja, mwendelezo, na mshikamano kwa Agano la Kale na Agano Jipya, na hakuna anayeweza kudai kuwa na mtazamo kamili au sahihi kuhusu Biblia bila Yeye – Kristo – kuwa kiini katika hatua zote za ufasiri. Yeye ndiye mada ya Biblia (Yohana 5:39-40). Katika somo letu la tatu, Ushahidi wa Agano la Kale kuhusu Kristo na Ufalme Wake: Kutolewa kwa Ahadi , tutachunguza uhusiano kati ya Agano la Kale na Agano Jipya kupitia dhana ya ufunuo endelevu . Tutaangalia miunganiko ya ziada iliyopo katika Agano la Kale na Agano Jipya jinsi inavyohusiana na nafsi ya Kristo na Ufalme wake, na kuzingatia mada ya pekee ya ahadi na utimilifu , na jinsi mada hii inavyoliunganisha fundisho la Maandiko kuhusu Yesu Kristo na kulifanya kuwa moja. Umoja huu wa kweli unaonekana katika ahadi ya Mungu ya ajabu ya kutuma mkombozi kwa wanadamu ambaye kupitia kwake adui wa Mungu angeangamizwa, na wanadamu wangekombolewa. Katika protoevangelium (yaani, tangazo la kwanza la Injili katika Mwanzo 3:15), kupitia ahadi ya agano la Ibrahimu na mwendelezo wake tunaona jinsi tumaini la Kimasihi ndio kanuni unganishi ya Agano la Kale na utimilifu maridhawa wa Agano Jipya, huku kilele cha yote kikipatikana katika Yesu Kristo. Yeye ni uzao wa mwanamke na uzao wa Ibrahimu. Maandiko ya Kiebrania na yafunue utukufu wake kwetu, na kutugeuza tunapokuwa wanafunzi wenye bidii wa Neno takatifu la Mungu! Ni dhahiri kwamba somo muhimu zaidi na lenye maana zaidi katika maisha ya kiongozi wa Kikristo ni kujifunza kumfahamu Yesu Kristo wa Nazareti na mafundisho yake. Hakuna somo lingine lililo muhimu au lenye utata kama maana ya maisha na huduma yake. Katika somo letu la nne, Ushahidi wa Agano Jipya kuhusu Kristo na Ufalme Wake: Kupingwa kwa Masihi , tutachunguza dhana ya Kiyahudi ya Ufalme wa Mungu wakati wa Yesu. Tutaona jinsi taifa la Israeli, lililokandamizwa na dola za kisiasa, liliamini kwamba Masihi atakapokuja, Ufalme wa Mungu ungekuja kwa nguvu, kuleta urejesho wa ulimwengu unaoonekana na kuokoa wanadamu kutoka katika udhibiti wa Shetani. Bila shaka, Yesu aliutangaza Ufalme kama uliokuwapo tayari, na alionyesha uhalisi wake katika uponyaji wake na kutoa pepo, akifunua kuwapo kwa Ufalme katika nafsi yake na huduma yake. Ni kweli, kuna uwezekano mkubwa kwamba kina cha huduma na uongozi wetu hakiwezi kwenda zaidi ya kina cha ujuzi wetu juu ya Yesu Kristo, Masihi wa Mungu na Bwana wa wote. Kwa sababu hiyo, Mungu wetu na Baba akupe wewe njaa, shauku, na nidhamu ili upate kuwa na ufahamu mahiri wa maisha na

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker