Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

84 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

kulipata. Hakuna kitu duniani kinachodumu kama hicho; hakuna kinachoweza kutupatia hekima, ufahamu, tumaini, na shangwe ambayo Neno linatoa. Neno la Mungu ni mali yenye utajiri mwingi, hutia macho nuru, hufurahisha moyo, huhekimisha nafsi, na kuleta tumaini katika maisha ya mtu. Mtunga-zaburi hapa anaonyesha wazi jinsi Neno lililo hai la Mungu linavyostahili kutamanika kwetu. Hakuna kitu ambacho tunamiliki au ambacho tunaweza kumiliki chenye thamani na umuhimu kama Neno la Mungu kuhusu Mwana wake, mpango wake, na tumaini letu. Katika kulishika tunaonywa, na katika kushikamana nalo kuna thawabu makubwa. Je, unatafuta Neno la Mungu kama vile unavyotafuta pesa, au raha, au muda huru wa kujiburudisha, au nafasi kubwa? Hakuna kitu katika ulimwengu huu chenye thamani au umuhimu kama ujuzi wa kina wa Neno la Mungu. Haja ya moyo wako iko wapi leo? Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni Imani ya Nikea (iliyo katika kiambatisho), sali sala zifuatazo: Mungu wa Milele, Baba yetu, tunakusifu kwa nia yako ya kujidhihirisha kwetu kupitia Neno lako. Umetubariki kwa kuhifadhi ahadi yako ya neema na matamko yako kwa njia ya Maandiko, ambayo uliyavuvia kwa Roho wako Mtakatifu. Na sasa, kwa njia ya Roho huyohuyo, unatufundisha kuhusu Mwana wako, na mpango wako mtukufu wa kurejesha vitu vyote ndani yake. Tunavyolibariki jina lako kuu na takatifu kwa Neno lako lililo hai na la kudumu, na tunakuomba utujalie hekima yako tunapojifunza pamoja nguvu na ukuu wa Neno lako. Mungu mwenye rehema, Baba wa mbinguni, umetuambia kwa kinywa cha Mwanao mpendwa, Bwana wetu Yesu Kristo, “Mwombeni Bwana wa mavuno,” juu ya agizo lako hili la kimungu, tunaomba kutoka mioyoni mwetu, kwamba umtoe Roho Mtakatifu kwa wingi kwa watumishi wako hawa, pamoja nasi na wale wote walioitwa kulitumikia neno lako. Amina.

1

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi Ukurasa wa 70  4

M A S O M O Y A B I B L I A

~ Martin Luther. Ibada na Maombi ya Martin Luther. Trans. Andrew Kosten. Grand Rapids: Baker Book House, 1965. uk 77.

Hakuna Maandiko ya kukariri somo hili.

Uhakiki wa Kukariri Maandiko

Hakuna kazi katika somo hili.

Kazi za Kukusanya

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker