Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | UONGOFU NA WI TO : NENO L I NALOUMBA / 97
ndani ya mwamini ukomavu wa kiroho, kina, na ukuaji katika kusudi na mapenzi ya Mungu.
Iwapo ungependa kufuatilia baadhi ya mawazo ya Neno Linaloumba , unaweza kujaribu vitabu hivi: Fee, Gordon D. na Douglas Stuart. How to Read the Bible for All Its Worth . Grand Rapids: Zondervan, 1982. Montgomery, John Warwick. God’s Inerrant Word . Minneapolis: Bethany Fellowship, 1973. Sproul, R.C. Knowing Scripture . Downers Grove: InterVarsity, 1977. Tenney, Merrill. The Bible: The Living Word of Revelation . Grand Rapids: Zondervan, 1968. Sasa ni wakati wa kujaribu kukazia somo lako la Nguvu ya Uumbaji ya Neno la Mungu kwa kulihusianisha na muktadha halisi wa kihuduma ambao unakabiliana nao au umewahi kukabiliana nao, na ambao utatumia muda kuufikiria na kuuombea katika wiki hii yote ijayo. Je, ni kwa jinsi gani hasa nguvu ya uumbaji ya Neno la Mungu inahitaji kudhihirishwa katika maisha na huduma yako wiki hii? Je, umepata maarifa fulani katika somo hili ambayo yanahitaji kusisitizwa katika kile unachofanya katika huduma yako kanisani? Ni dhana gani hasa ambayo Roho Mtakatifu amekuonyesha ambayo unahitaji kuielewa vizuri zaidi, au jambo ambalo unapaswa kuchukua ili kujifunza kwa undani zaidi? Tafakari mbele za Bwana kwa muda na umwombe akufunulie hasa jinsi unavyoweza kufafanua kwa kina zaidi ukweli huu kwamba Neno lake ni Neno linaloumba, katika kanisa lako, familia yako na maisha yako. Mwombe Mungu Roho Mtakatifu auangazie moyo wako kuhusu nguvu zinazotoa uzima na uwezo wa kiungu ambao hulihuisha na kulijaza Neno la Mungu. Mwombe Mungu akupe ufahamu mkubwa zaidi wa maana ya Neno la Mungu, na akupe muda mwingi na mzuri zaidi wa kutumia kwa ajili ya kusoma, kujifunza, kukariri na kulitafakari Neno katika maisha yako katika wiki hii. Omba pia kwamba Mungu afanye mahubiri na mafundisho yanayotolewa katika kanisa lako yawe hai kwako unaposikiliza na kutafakari kweli hizi. Zaidi ya yote, mwombe Mungu akutumie zaidi na zaidi kama mwalimu wa Neno la Mungu aliyefundishwa na Roho ili kumfunua Mungu na kusudi lake kwa uwazi zaidi kupitia mafundisho yako. Kadiri unavyolielewa Neno la Mungu vizuri zaidi, ndivyo linavyoingia ndani ya nafsi na akili yako na kukuathiri, na
Nyenzo na Bibliografia
1
Kuhusianisha Somo na Huduma Ukurasa wa 72 10
M A S O M O Y A B I B L I A
Ushauri na Maombi Ukurasa wa 72 11
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker