Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
96 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Neno la Mungu kwa mujibu wa King James wa Uingereza Katika moja ya ushemasi wa kanisa kumetokea mabishano makubwa katika kipindi cha mafunzo ya Biblia ya nyumbani kuhusu tafsiri gani za Biblia zinafaa kutumiwa. Kikundi kimoja cha waamini wazee kimedai kwamba Biblia pekee inayopaswa kutumika katika kundi hilo ni Biblia ya King James, tafsiri iliyothibitishwa na ya kweli ambayo kwa muda mrefu imeheshimiwa na kuthaminiwa kanisani. Kundi la vijana wanasisitiza kutumia baadhi ya tafsiri za “kisasa”, kwa sababu wanaona ni rahisi sana kusoma na kukariri. Kwa wale wa kundi la watu wazima, mistari inaposomwa kutoka katika tafsiri mpya zaidi, wanahisi kana kwamba maana nzima ya mstari huo imebadilika. Pande zote mbili zinajua kwamba Biblia haikuandikwa awali katika Kiingereza, lakini hakuna hata mmoja katika makundi yote mawili anayeelewa Kiebrania au Kiyunani. Kama mchungaji, unawezaje kutatua tatizo hili katika ushamasi huu? Unamhitaji Roho Mtakatifu Baada ya kusikia fundisho kwenye televisheni lililosema kwamba hakuna mtu anayeweza kuielewa Biblia bila msaada wa Roho Mtakatifu, shemasi mmoja kanisani anahangaika sana kwa habari ya kutoelewa kwake Biblia. Ingawa anaelewa kwamba Roho Mtakatifu alikuja na kukaa ndani yake na kumtia muhuri mara tu alipoamini (k.m., Rum. 8:1-18; Efe. 1:13; Gal. 5:16-23), hajui maana ya “kufundishwa” na Roho takatifu. Haamini sana kwamba anapaswa kupitia mazoezi mengi ya kihisia ili kusema kwamba anafundishwa na Roho, na kila mtu anamtambua ndugu huyu mpendwa kuwa ni mtumishi aliyekomaa, mcha Mungu, na mwenye kumfanania Kristo katika kanisa. Bado, anataka kuelewa maana ya kufundishwa na Roho. Je, ungewezaje kumfundisha ndugu huyu kuelewa utendaji wa huduma ya kufundisha ya Roho Mtakatifu katika jitihada zake za kuendelea kujifunza Biblia? Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu, rekodi iliyoandikwa ya Neno la Bwana lenye uzima na la milele. Kwa sababu yamevuviwa na Roho Mtakatifu (kihalisi, pumzi ya Mungu) ni ya kuaminiwa kabisa na ya kutegemewa katika yote yanayosemwa ndani yake. Neno la Mungu hutupatia kusudi la Mungu la milele juu ya uumbaji, yaani, kwamba vitu vyote vilifanywa kupitia Neno la Mungu liumbalo na linalotoa uhai kwa utukufu wake mkuu. Bwana Mungu anajitambulisha kikamilifu katika Neno la Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye ndiye ambaye kupitia kwake Mungu anajifunua kwetu, anaukomboa ulimwengu, na atarudisha ulimwengu wote chini ya utawala wake wenye adili. Neno hili, kwa njia ya Roho Mtakatifu, hutengeneza maisha mapya ndani ya wale wanaoamini. Ufuasi wa kweli ni kudumu katika Neno hili katika Kanisa, ambalo huzaa
3
1
M A S O M O Y A B I B L I A
4
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker