Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 0 1
Mt. 14:23-25 – Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. 24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho. 25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Mk. 6.46 – Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba. Kol. 4:2 – Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani. Pia, usichukulie kuwa ni jambo la kawaida sana au lisilo la lazima kuwauliza wanafunzi kama wanahitaji maombi kwa ajili ya mtu fulani au kitu kinachohusiana na mawazo na kweli zinazofundishwa katika somo. Maombi ni njia ya ajabu ya kutumia kweli kwa njia ya vitendo na yenye manufaa; kupitia kupeleka mahitaji maalum kwa Mungu kwa kuzingatia ile Kweli ya Neno la Mungu, wanafunzi wanaweza kuimarisha mawazo hayo katika nafsi zao, na kupokea tena kutoka kwa Bwana majibu wanayohitaji ili kutegemezwa katikati ya huduma zao. Bila shaka, kila kitu kinategemea kiasi cha muda ulio nao katika kipindi chako, na jinsi ulivyoupanga. Bado, maombi ni sehemu yenye nguvu na yenye uwezo wa kukutana na mafundisho yoyote ya kiroho, na kama unaweza, yanapaswa kuwa na nafasi yake kila wakati, hata ikiwa ni maombi mafupi ya yale ambayo Mungu ametufundisha, na azimio la kuishi kulingana na matokeo yake kama Roho Mtakatifu anavyotufundisha.
4
M A F U N Z O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online