Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 0 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Kilicho muhimu kusisitiza hapa ni kwamba kuja kwa Masihi kulihusiana moja kwa moja na kuyashinda majeshi ya pepo wabaya, pamoja na zile athari za laana na nguvu za uovu ambazo zilitaka kuingilia uthibitisho wa utawala wa Mungu juu ya uumbaji wake.
Mifano hii imeundwa ili kuibua majadiliano na mazungumzo ya wazi kuhusu baadhi ya athari zinazohusiana na maoni ya kisasa ya mateso, upinzani, migogoro, na ushindi katika maisha ya Kikristo. Kilicho muhimu kuzingatiwa hapa ni kwamba masuala haya ni baadhi ya mambo ya kawaida na yaliyoenea sana katika Kanisa, hasa katika kanisa la Marekani ambalo lina mwelekeo wa kufikiria ushindi wa Kristo katika misingi ya afya, mali, na baraka. Mtazamo huu wa maisha ya Kikristo ni wa kawaida sana kiasi kwamba wengi wanauchukulia kuwa ndio usomaji na tafsiri pekee ya kuaminika ya maana ya maisha na kifo cha Kristo kwa ajili yetu leo. Kupitia tena swali hili ni muhimu, hasa kwa wale wanaopanda makanisa na kufanya wanafunzi katika vitongoji miongoni mwa watu maskini, walionyimwa haki, waliofilisika na wenye mazingira hatarishi. Wahimize wanafunzi wako kushughulika na dhana hizi, kwa kuwa ziko chini ya kada nzima ya masuala yanayohusiana ambayo yanaibuka kutoka katika mifumo tofauti ya kiroho ya Kikristo ambayo waamini wanaifuata leo. Katika somo hili, ambalo linaangazia maswala ya mateso, upinzani, na migogoro, inapaswa kuwa wazi kwamba msisitizo wa maombi unafaa. Ukiweza, tafuta kutumia muda mzuri katika somo hili juu ya maombi, hasa kwa vile hii ilikuwa njia ya hakika na ya kawaida ya Yesu ya kupokea kutoka kwa Baba neema, maelekezo, na uongozi aliohitaji ili kustahimili mashambulizi ya mara kwa mara ya maadui zake wa kidunia na maadui zake wasioonekana. Katika hili, tunapaswa kuiga mfano wa Kristo na Mitume, ambao walifanya maombi kuwa nidhamu muhimu na endelevu katika maisha yao. Lk 6:12-13 – Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 13 Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume.
6 Ukurasa wa 174 Mifano Halisi
4
M A F U N Z O Y A B I B L I A
7 Ukurasa wa 177 Ushauri na Maombi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online